Inaonekana umekwishafikia hitimisho kwamba wazazi ndio wenye matatizo. Hivyo wazazi ndio wanabidi wajirekebishe.
Kutoelewana baina ya wazazi na watoto kunatokana na sababu nyingi tofauti. Zipo ambazo zipo wazi na jamiii inaweza amua bila wasiwasi ni nani mkorofi. zipo sababu ambazo haziko wazi hivyo ni vigumu kwa jamii kuhitimisha ni nani mkorofi.
Binafsi naungana na wadau waliosema kutojibishana na wazazi ni jambo bora, hata kama wewe mtoto unaamini unahaki.
Zamani koo katika nyingi walikuwepo wazee ambao mtoto anapokosewa na mzazi mtoto alikuwa anaweza kwenda waona hao wazee na kuwasilisha malalamiko yake. Wazee hawa walikuwa na mbinu ya kufikisha ujumbe kwa mzazi bila ya mzazi kuona kakosewa heshima. Mzazi alikuwa haombi msamaha ila harudii tena lile kosa (japokuwa walikuwepo wazazi wakorofi ambao kwenda kwa wazee hawa ilikuwa kama unawachochea moto). Mfumo huu umepotea, hivyo kwa sasa ukimya ni njia madhubuti ya kuepuka ugomvi na wazazi.
Wanaosema umpotezee mzazi, mkumbuke kwamba nanyi mkijaaliwa mtakuwa na watoto. Hawa watoto watakuwa wamelelewa katika mazingira ya kutoona umuhimu wa kuwa karibu na wazazi wanapokuwa wakubwa (wameona jinsi babu na bibi yaowalivyopotezewa na maisha yakasonga bila tatizo) hivyo na wao wakiwa wakubwa hawataona shida kuwapotezea wazazi wao (wakipata hata sababu ndogo tu).
Mhesshimiwa,
TUnaongelea mazingira ya sasa na mazingira yanayoleta tatizo.
Ni kweli hitimishoa langu kwamba wazazi wakorofi. Nimefikia hitimisho hilo ili jamii kukabiliana na hili tatizo na nimeonye kwamba zamani nilidhani ni wachache kumbe linaongezeka na hivyo wewe changia jinsi ya kuliondoa.
Sijawahi na sitarajii kusikia eti mtafaruku ambao mtoto anayejitegemea kamkosea mzazi halafu hiyo ikawa ni issue nzito ikashindikana na jamii. Mtoto kumkosea mzazi si issue nzito ya kujadili maana mtoto atashambuliwa kila kona na hata mimi nitamshambulia.
Taabu ilivyonifanya nikaandika kama mna majibu msaidie ni pale mzazi ni mkorofi, tena si mkrofi tu, bali ni mkaidi. Ukaidi wa mzazi huja hasa anapotambua kwamba ana washabiki wengi kwenye jamii kwa hiyo mifano niliyoona ni ile ambay watoto wameona potelea mbali wingi wa washabiki anaamua kufanya niliyosema na nimeona yakiwafika wazazi wengi ambao sipendi yazidi kuwafika.
Ninataka wazazi wazidi kupendana na watoto wao hadi kifo chao na ndiyo maana ninaleta msaidie kuliko kuchochea moto kama baadhi yenu ninavyowaona.
mfumo unaousema wa wazee kumkanya kimyakimya nao tunaujua na sikuutaja kwa sababu umeshapitwa na wakati. Mfumo huo luifaulu labda kwa waliozaliwa nyuma ya mwaka 1960 ambako wengi walizaliwa na kuishi vijijini.
Wengi sasa tumezaliwa mjini ambako jirani yako si tu ni kabila jingine, bali jirani yako ni mwingereza au mmarekani. Huwezi kutegemea mfumo wa zamani kutatua tatizo hili kwa maisha yaliyobadilika namna hii.
Ndiyo maana nasisitiza tusiendelee kudekeza wazazi wakorofi wakati madhara ya ukorofi wao yanaweza kuleta kilema kikubwa cha maisha.
Wapo nilioona wakipigika kwa kufuata wazazi wao na waliotupilia mbali wazazi wakorofi wakainuka kimaisha.
Tusidanganyane, tutafute suluhisho linaloleta haki na tusimwonee aibu mkorofi hata kama ni mama au baba.