Kukosana na mama au baba mzazi ni Janga jipya kwenye jamii. Tulifanyie utafiti. Tusikurupuke

Mkuu kweli uzi wako umejaa ukweli mtupu,,,mimi ni mhanga mkubwa wa hilo tatizo lakin hakuna mtu amewahi kunielewa kila mtu anasimama upande wa mzazi,,wachache tu humu Jf ndo walinielewa na kunipa ushauri ila kwa jamii ya huko mtaan inayonizunguka hakuna hata mmoja anaeelewa situation yangu
 
Hii thread ni wachache sana ambao wanaweza kuielewa....ukiacha waliopatwa na mikasa hii na walioshuhudia mikasa ya aina hii, wengi wao watashindwa kuelewa unazungumzia nini. Binafsi nakuelewa sana mkuu na nimesubscribe kabisa kuufuatilia kwa ukaribu
 
Mkuu asante kwa kuleta uzi mzuri, nakubaliana na ww kabisa kwamba kuna baadhi ya wazazi bado wanadhani wako enzi zao za miaka ya 80 kurudi nyumba

Mzazi/wazazi wana wajibu wa kuwalea watoto wao katika maadili mema tokea wadogo hadi wakubwa, ila kuna umri watoto wao wakifika hujitegemea

Sasa unapokuwa tayar mtu mzm unajitegemea halafu wazazi bado wanataka wakufanyie baadhi ya maamuzi yanayohusu mustakali wa maisha yako ndio matatizo huanzia hapo

Ni lazima wazazi wajifunze kuwa kwa sasa kuna mabadiliko makubwa ya kimazingira ya miaka ile na ya sasa na vijana wa sasa wanachangamoto nyingi na tofauti na za enzi zao

Kwa hiyo wao wanapaswa kuwa washauri tu na sio kulazimisha mambo kwa watoto wao ili kuepusha ugomvi usio wa lazima baina yao na watoto wao

Kwa mf unakuta mzaz/wazazi wanamlazimisha mtoto asomee course fulan wakati kijana wao kila siku yuko mtandaoni na anaona changamoto za ajira za hiyo fani, au wanamchagulia kijana wao mke/ mme hata kama hamtaki eti ukubali tu kisa wazazi watakuachia laana, ama watoto wamependana wao wanakataa ndoa ifungwe huku wakiweka vigezo vyo visivyo na mashiko kama kabila, dhehebu, rangi, urefu ama ufupi/ unene ama wembamba, elimu n.k

Hivyo wazazi wanapaswa kuheshimu mawazo ya vijana wao kwa kutambua wamekuwa na pia wana vipa umbele vyao

Pia watoto/ vijana wanapaswa kuwaheshimu wazazi na sio kuwadharau kwa kuwa labda wamewazidi elimu ama hali ya kiuchumi ila wanavyofanya maauzi mazito ya kimaisha kama ndoa ni vzr wakiwashirikisha walezi wao , ila isiwe ndio mwanya wa wazazi kuwa na final say
 

Hii thread ni wachache sana ambao wanaweza kuielewa....ukiacha waliopatwa na mikasa hii na walioshuhudia mikasa ya aina hii, wengi wao watashindwa kuelewa unazungumzia nini. Binafsi nakuelewa sana mkuu na nimesubscribe kabisa kuufuatilia kwa ukaribu

Wakuu,

Hata ukisoma makala ya leo ya GENERALI ULIMWENGU kwenye RAIA MWEMA ya leo, anasema kitu hikihiki.

Nashukuru wanaoelewa kwani siku zote ukiwa muelewa maana yake una experience na unaweza kuokoa situation, tofauti na wajinga waropokaji.
 
Mkikaa pamoja pamoja mifarakano ya familia haikosi. Ndiyo maana wenzetu mtu akifika miaka 18 anaondoka nyumbani kuanza kujitafutia maisha yake. Hapo wazazi watam miss motto na motto atawa miss wazazi.
 
Yamenikuta hapo kwenye kuchaguliwa course na mzazi hata hajasoma🙂🙂.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…