Kukosea kuoa ama kuolewa umeharibu maisha

Kukosea kuoa ama kuolewa umeharibu maisha

General Nguli

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2022
Posts
1,190
Reaction score
2,508
Wanajamvi natumai kwema kwa wote hata mimi pia.

Naomba kuuliza huu msemo wa kukosea kuoa ama kuolewa umeharibu maisha; Kimtazamo umekaaje...?

Mfano;Mimi nina mke 1, na mtoto 1, nina miaka 5 ktk ndoa na Umri wangu 33. Nimeona kila Dalili kua nimekosea kuoa. Ikitokea nimejiengua katika hii ndoa ina maana future yangu na yenyewe itakuwa imearibika..???[emoji23]

Naombeni Muongozo ili nijifunze hatua za kuchukua japo ndoa lazima ivunjike na hakuna mjadala. Nawasilisha.

NB;Vijana wa kiume mnao taka kuingia kwenye ndoa kuweni makini sana. Chunguzaneni na hata mpimane Afya ya akili na sio Damu pekee.
 
Inamaana ukioa au kuolewa na ambae ni mruka Kwa uongo Hapa Lazima utaelewa maana ya huo msemo
 
Future yako inawezekana kuharibika kama kuna ule mgawanyo wa mali katika kutengana. Umehustle miaka 5-6 umenunua kiwanja umejenga now unaitwa baba mwenye nyumba.lakini mkigawana mali unaenda kuanza maisha upya.unarudi geto kama msela wa enzi zilee[emoji38][emoji38][emoji13] Unaanza harakati upyaa... Na bado malezi yanakungoja.

Nb:inategemea na ukubwa wa mgao mtaopeana.wengine wanagawana mil 500 Wengine mil 2 Wengine tunagwana suguria na mabakuli na makochi[emoji38]
 
Kwa nini future yako iharibike ikiwa hujaifikia hiyo future. Ishi sasa kama umeamua kuacha acha mtu maisha yaendelee.

Una anticipate future ambayo inaweza kukupa uongo au ukweli ambapo ukakifanya ushindwe kufanya maamuzi
 
Gen bado tuko kwenye tafiti kwanini mnayakwaa mabomu ya kutega. Ripoti kamili itakuja na tamko kuwa ulishaharibu kabla ya kuumiliki uharibifu na zaidi watoto si ajabu wakaangukia ulipo angukia wewe.
Naomba kuwasilisha.
 
Sehemu tatu za maisha: 1. Kuzaliwa 2. Kuoa au kuolewa 3 Kifo: Hiyo ya pili ndio mtihani mkubwa, ukikosea tu unaingia sehemu ya tatu chapchap. Nawashauri vijana muwe macho, muda wa uchumba uwe mrefu ili mchunguzane.
 
Kweli ukikosea kuoa jua umekosea na maisha.
Nakushauri ukae chini na mkeo myatengeneze kabla hayajaharibika mazima.
 
Sehemu tatu za maisha: 1 kuzaliwa 2 kuoa au kuolewa 3 kifo: Hiyo ya pili ndio mtihani mkubwa, ukikosea tu unaingia sehemu ya tatu chapchap. Nawashauri vijana muwe macho, mda wa uchumba uwe mrefu ili mchunguzane.
Kabisa kaka... Wengi tunauvagaa kwakuangalia mapaja na rangi.
 
Future yako inawezekana kuharibika kama kuna ule mgawanyo wa mali katika kutengana.
Umehustle miaka 5-6 umenunua kiwanja umejenga now unaitwa baba mwenye nyumba.lakini mkigawana mali unaenda kuanza maisha upya.unarudi geto kama msela wa enzi zilee[emoji38][emoji38][emoji13]
Unaanza harakati upyaa...
Na bado malezi yanakungoja.

Nb:inategemea na ukubwa wa mgao mtaopeana.wengine wanagawana mil 500
Wengine mil 2
Wengine tunagwana suguria na mabakuli na makochi[emoji38]
Bora kuanza upya kuliko kuwa mtumwa na usie na furaha na maisha yako yote.
 
Kwa nini future yako iharibike ikiwa hujaifikia iyo future. Ishi sasa kama umeamua kuacha acha mtu maisha yaendelee.

Una anticipate future ambayo inaweza kukupa uongo au ukweli ambapo ukakifanya ushindwe kufanya maamuzi
Asante kaka...
Kuliko kuishi na mwanamke asie jitambua akili na hata maisha kwa ujumla.
 
Siku zote future ya watu wote dunia hii ni nzuri

Ila mipango yako ya leo ndio itaharibu au kutengeneza future ya kesho
 
Ni hatari sana ukikosea kuoa utajuta yaani.

Mfano muachane ghafla Kuna gharama kubwa sana huwezi kujua kama malezi ya watoto kama kweli una akili hapo unafikiria na future ya mtoto kama utaoa akienda kukaa kwa mama wa kambo (mkeo mpya) hapo atanyanyasika ..Bado akienda kwa mama ake mzazi kule utatuma pesa kama Kuna Mali zitagawanywa .

Kuna mtu namfahamu alioa mwanamke wa huko chuo yeye wa nyumba ila mke wa huko kaskazini mtoto mmoja ila jamaa hamuelewi mke kabisa mpaka ujenzi kaacha Bora akalewe maana anaona Kuna taa nyekundu mke anataka gharama na kila kitu kipelekwe kwao haswa December anaweza kutaka hata mil 5 aende nazo kwao😂...Jamaa kasema hawezi kujenga maana wanaweza kulipuana mda wowote Bora pesa afiche au akalewe tu
 
Kwani umekuja duniani for the sole purpose of kuoa? If yes then yes umeyaharibu maisha...
 
Haiharibiki inategemea mmeoana iki iweje kama kujenga familia haiharibiki hata

Ishumambo ya mali make sure unasema lugha moja na mkeo othawais u a in big trabo
 
Mkuu mtoa mada humu tunatumia ID fake. Mimi natamani uziseme changamoto ulizobaini kwa mkeo. Yawezekana kabisa kuna wana jf walizipitia na kuna njia walizotumia kuzitatua na ndoa zao zikapona kabisa. Kupishana kitabia kwa wanadoa ipo maana kila mtu amezaliwa familia tofauti na ya mwenzie. Kila mwanandoa amepata makuzi tofauti na mwenzie...so kuna kutofautiana kwingi tu. Na pia hakuna mtu yuko perfect 100% labda umuumbe wewe. Yawezekana mkeo naye anaona wewe una mapungufu fulani....nini kifanyike.....weka shida ulizoziona kwa mkeo jf ni pori. Hutakosa mazuri ya kuondoka nayo. Yawezekana kuna shida kubwa na ndoa haitowezekana kupona utajua hapa hapa . Au ni changamoto za kutatulika pia utajua. Mwisho mtwishe Mungu fadhaa zako naye atakufanyia wepesi.
 
Back
Top Bottom