Ukweli ni kwamba, mwanadamu ana mipaka ya uwezo katika utendaji wake; yani mwanadamu ana mapungufu katika namna moja ama nyingine, hivyo kushindwa kufanya mambo fulani kwa ukamilifu- hivyo hukosea (au kufanya makosa).
Na hili ni dhahiri katika nyanja zote tu zinazohusu maisha ya mwanadamu: kijamii, kiuchumi, n.k.
Mara nyingi inapotokea mtu amefanya kwa kukosea, kinachoweza kuja haraka sana ni hali ya kujisikia hasi (sense of negativity) kwamba siko makini, au sina ufahamu wa kutosha, au napungukiwa vitu fulani vizuri na hapa tayari nimepata hasara, labda ningekuwa na uwezo kama fulani basi nisingekosea hivi.
Ni kweli kwa sehemu kila mmoja wetu anaweza fika kujisikia hivyo; lakini pokea ushauri huu leo mwenzangu, usidumu kwa muda mrefu katika kujisikia hivyo, simama haraka, jikung'ute mavumbi ya makosa yako na usonge mbele zaidi maana KUKOSEA NI DARASA LA KUVUNA FAIDA PIA, kukosea kwako leo ni faida yako ya baadaye katika enoe fulani la maisha yako, linaweza kuwa hilo ama lingine tofauti.
Katika andiko hili napenda tuone jinsi gani tunaweza pata faida katikati ya yale tunayokosea; kwa kusema hivyo simaanishi kwamba natukuza makosa(ya uzembe) la hasha! Ila badala yake natamani kuona wengine pia(kama mimi) wakifanya vizuri tena na zaidi hata baada ya kufanya makosa fulani katika maeneo fulani ya maisha, maana kukosea siyo mwisho wa kushindwa kuendelea mbele.
Naomba zingatia mbinu zifuatazo pale unapokutana na hali ya kukosea katika nyanja fulani ya maisha yako:
• Litambue Kosa lako:
Hii ni hatua ya kwanza na muhimu kabisa; tambua ni wapi ulipofanya kwa kukosea, bila kutambua tulipokosea hatutaweza kabisa kurekebisha makosa, badala yake tutaendelea kutembea katika njia ya kukosea zaidi. Kwahiyo, pata muda, tuliza ufahamu wako(tafakari) kulitambua kosa lako katika eneo fulani.
• Tambua Visababishi vya Wewe Kukosea:
Katika kila kosa kuna visababishi vilivyopelekea, inaweza ikawa ukosefu wa maarifa fulani, au tabia fulani za mtu binafsi, au sababu zingine kabisa ambazo yamkini ni nje kabisa na sisi wenyewe. Ni nzuri kuzitambua. Sio tu kuzitambua ili kuziondoa(maana zingine hazitaondoka), ila angalau unakuwa na ufahamu jinsi ya kukabiliana nazo zinapotokea wakati mwingine, kama ni zile zisizoondoka kabisa.
• Tembea kwa Umakini zaidi:
Kama nilivyosema awali, wanadamu tuna mapungufu yanayotuzuia kufanya kwa ukamilifu, hivyo wote kwa namna fulani tunakosea. Ninaposema, "kutembea kwa makini", natumia hii kama lugha ya picha, ni kama vile mtu anatembea kuelekea mahali fulani kupitia njia fulani yenye mawe, ambayo anaweza kujikwaa(ndiyo kukosea) hivyo basi umakini unahitajika. Katika umakini huu, sio kwamba tutaondoa hali ya sisi kukosea, hapana!, ila angalau hatutajikosesha kwenye namna ile ile ya makosa iliyotukwamisha kuendelea mbele wakati fulani, mathalan kwenye masuala ya maendeleo.
Ni matumaini yangu tafakari hizo chache, zitakuwa zimetusaidia kwa namna fulani;
Usijihukumu unapokosea, jisamehe pia. Kumbuka wewe sio mkamilifu, utafanya kwa kukosea tu kwa namna fulani. Cha msingi ni kusonga mbele.
Alishawahi sema mtu mmoja, "haijalishi unatembea, unakimbia au unatambaa. Cha msingi wewe songa mbele", hii iwe hamasa yetu wote leo, kwamba shabaha yetu iwe ni katika kusonga mbele, kusonga mbele kijamii, kiuchumi, na kwa mambo yote mema na ya maendeleo, bila kujali tunakosea mara ngapi.
Katika kila kukosea kuna kujifunza upya, hakika kukosea ni darasa la kuvuna faida pia, kukosea siyo mwisho wa safari yako ya maendeleo. SONGA MBELE ZAIDI kuliko ulivyoanguka jana kwa kukosea.
Asante sana Kwa Kusoma
KARIBU KWA KUPIGA KURA.

Upvote
6