The English words that best translate 'ulegevu' are laziness, sloth, idleness, negligence, and indolence.Nimeona mada nyingi hapa JF zina makosa ya tahajia (spelling) za maneno ya Kiswahili. Na watu hawaoni kuwa hilo ni tatizo. Matatizo wanayoona ni ya kisiasa! Hii ni dalili ya ulegevu wa kiakili, kutokujali na kukosa bidii ya kujifunza lugha.
Lugha ni zana ya hekima na ufanisi. Mtu anayeijua lugha yake vizuri anaeleweka kwa urahisi na hupewa heshima. Ukikosea tahajia mara kwa mara, hasa kwa maneno ya kawaida, unadhihirisha kuwa huna bidii ya kazi, hupendi kujitahidi. Na hii ni ishara kwamba hata ofisini kwako au kwenye biashara yako unafanya makosa na hujali.
“Je! Umemwona mtu aliye mstadi katika kazi yake? Atasimama mbele ya wafalme, hatasimama mbele ya watu wa kawaida.” (Methali 22:29)
Andiko hilo linaonyesha kuwa ustadi, hata katika kuandika, huinua mtu. Kinyume chake, mtu mlegevu hata kufanya "proof-reading" hastahili cheo kikubwa.
"Lolote mkono wako upatalo kufanya, fanya kwa nguvu zako zote, kwa kuwa huko kuzimu, unakoenda, hakuna kufanya kazi wala mipango wala maarifa wala hekima.”
Kama unaandika mada, andika kwa bidii. Zingatia tahajia sahihi.
Methali 18:9
"Mtu mvivu kazini mwake ni ndugu yake mharibifu.”
Kukosea tahajia sio jambo dogo; ni ulegevu unaoweza kuharibu mawasiliano na kuathiri picha yako mbele ya watu. Mmenipata, wakuu? Ni Injili tu kila kona! 😎
Kauli hutamkwa.Haiandikwi.Uzi unakuhusu.Sikutegemea mtu kama wewe unaweza kutoa kauli hii!
Umetumia neno " huna" na neno "hupendi", nieleze usahihi wa maneno hayo badala ya "hauna na haupendi".Nimeona mada nyingi hapa JF zina makosa ya tahajia (spelling) za maneno ya Kiswahili. Na watu hawaoni kuwa hilo ni tatizo. Matatizo wanayoona ni ya kisiasa! Hii ni dalili ya ulegevu wa kiakili, kutokujali na kukosa bidii ya kujifunza lugha.
Lugha ni zana ya hekima na ufanisi. Mtu anayeijua lugha yake vizuri anaeleweka kwa urahisi na hupewa heshima. Ukikosea tahajia mara kwa mara, hasa kwa maneno ya kawaida, unadhihirisha kuwa huna bidii ya kazi, hupendi kujitahidi. Na hii ni ishara kwamba hata ofisini kwako au kwenye biashara yako unafanya makosa na hujali.
“Je! Umemwona mtu aliye mstadi katika kazi yake? Atasimama mbele ya wafalme, hatasimama mbele ya watu wa kawaida.” (Methali 22:29)
Andiko hilo linaonyesha kuwa ustadi, hata katika kuandika, huinua mtu. Kinyume chake, mtu mlegevu hata kufanya "proof-reading" hastahili cheo kikubwa.
"Lolote mkono wako upatalo kufanya, fanya kwa nguvu zako zote, kwa kuwa huko kuzimu, unakoenda, hakuna kufanya kazi wala mipango wala maarifa wala hekima.”
Kama unaandika mada, andika kwa bidii. Zingatia tahajia sahihi.
Methali 18:9
"Mtu mvivu kazini mwake ni ndugu yake mharibifu.”
Kukosea tahajia sio jambo dogo; ni ulegevu unaoweza kuharibu mawasiliano na kuathiri picha yako mbele ya watu. Mmenipata, wakuu? Ni Injili tu kila kona! 😎
Kweli?Kwa hiyo ikiandkwa ..."NO DEFAULTS,NO ERECTION" itakuwa poa tu?Lengo kuu la lugha ni mawasiliano(kufikishiana ujumbe) hayo mambo ya spelling ni mbwembwe tu..
No reforms No election..
Hapa unaona uko sahihi??wanayoona
Asante sana Rodwell mTZHata wewe mwandishi wa huu Uzi,umeishapigwa bao moja hapo,badala yakuandika "mnayoyaona" umeandika "mnayoona" ,hivi mnayoona ni myama gani huyo? Ama kweli inabidi mtu ajitoe boriti jichoni mwake kabla ya kumtoa kibanzi Jirani yake😂😂😂
Mtu kama yeye? Unamfaham nje ya hapa? Mshauri aende wodi ya wagonjwa wa akili. Mtanishukuru baadae.Sikutegemea mtu kama wewe unaweza kutoa kauli hii!