Kukosekana kwa mawakala, kikwazo kuelekea soka la Kisasa

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Haina ubishi kuwa mawakala na mameneja wana mchango mkubwa kwenye kufanya michezo iwe biashara, kutoka kwenye mtazamo wa sasa ambapo soka letu bado lina sura ya ridhaa.

Kwa mujibu wa tovuti ya FIFA, mawakala waliosajiliwa na TFF (utaratibu ni kuwa vyama vya nchi husika husajili na kuwathibitisha mawakala, kisha FIFA kutumiwa majina) ni wanne pekee huku mtandao wa mawakalaa wa Fieldoo ukiwa na mawakala watatu pekee waliojisajili kutokea Tanzania.



Wapo mawakala ambao hawajasajiliwa na TFF lakini ni Watanzania na wanafanya kazi kwa maslahi ya nchi yetu na mara kadhaa tumewaona wakijishughulisha na wachezaji wa hapa ndani, mfano ni wakala wa Shomari Kapombe ambaye amesajiliwa Uholanzi.

Mawakala huhudumu kama mameneja na walezi wa wachezaji, huwajibika kuwashauri kuhusu mwenendo wao mchezoni na nje ya mchezo. Kama mchezaji atashindwa kuishi maisha ya nidhamu na kujitunza, hasara huwa kwa wakala maana mchezaji huyo atakuwa hauziki.

Ni rahisi sana kuwalaumu wachezaji, lakini kuna kundi ambalo halitekelezi wajibu wake ipasavyo, mawakala na viongozi ambao wanawajibika kuwaunganisha wachezaji na mawakala.

Faida ya kuwa na wakala haikomei kwenye usajili wa kwenda Uaya pekee, wakala anawajibika hata kwenye uhamisho ambao unahusisha vilabu vya ndani na kumsimamia mchezaji kwenye mikataba mingine anayoingia.

Bila kubadili mtazamo wetu juu ya nafasi ya mawakala/mameneja wa wachezaji, bado tutaenda na kurudi kisha kuishia kuwalaumu viongozi wetu wa soka ambao wapo kwa maslahi yao zaidi.


waione: dfk-agent, vanmedy
 
tanzania kiuhalisia hao mawakala na wote wanaosimama kutetea haki za wachezaji na mfumo mzima wa michezo ni kama wanapigwa vita ya kisirisiri...
rejea zengwe la kufungiwa kwa wakala/mwanasheria DAMAS NDUMBARO kutojihusisha na mchezo wa soka na tff..
on the other hand uwepo wa mawakala makini na waliosajiliwa haitokuja itokee issue kama ya singano .. Mphamvu
 
Last edited by a moderator:

Boi, huwezi kutetea haki ya mtu ambaye haijui... Tunatakiwa tuanze kuwaelimisha kwanza, waijui hiyo haki la sivyo akija laghai mwingine akimwambia anapotoshwa na wakala atamuamini.
 
Last edited by a moderator:
Boi, huwezi kutetea haki ya mtu ambaye haijui... Tunatakiwa tuanze kuwaelimisha kwanza, waijui hiyo haki la sivyo akija laghai mwingine akimwambia anapotoshwa na wakala atamuamini.

haya yanayowakuta sass (hii case ya wachezaji kutapeliwa mikataba).. NI ELIMU TOSHA.. kung'atwa na nyoka ni njia nzuri sana ya kutufanya tuuogope hata unyasi....
AUTOMATICALLY KAZI YA WAKALA TUTAIONA UMUHIMU WAKE KAKA.
juzi c.ronaldo kamzawadia wakala wake kisiwa kama zawadi ya harusi.. haitupati kama funzo hili kuwa hawa watu ni muhimu...
.
Mphamvu
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…