Kukosekana kwa wachezaji wa Man City kwenye FIFA Pro inamaanisha nini?

The real Daniel

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2017
Posts
2,117
Reaction score
7,899
Pamoja na kutwaa mataji yote ya england na kufika robo fainali ya UEFA bado hakuna mchezaji yeyote wa city kwenye kikosi bora cha dunia. Imagine hata benardo hayupo. Cha ajabu unakutana na wachezaji 4 wa Real madrid, timu ambayo haikuwa na msimu mzuri.

Mfano mtu kama marcelo alikuwa anapigwa benchi na kale ka regulion lakini yupo kwenye kikosi. Pia mtu kama mane kaupiga sana msimu uliopita lakini hayupo.

Mtazamo wangu kikosi kilichotangawa hakiakisi uhalisia kabisa
Screenshot_20190924-081745~2.jpeg
 
Man city mchezaji wa kuwepo pale labda ni Benardo silva.hasa ukizingatia kikosi ni kigumu kwenda mbele.But upande wa mabeki ndo FIFA wamezingua zaidi.Marcelo hafai kabisa kuna dogo Trent Arnod aliupiga mwingi sana ila hayupo.
 
Kweli kabisa, yaan dogo anold ameimfluence sana liver kuchukua ndoo ya uefa. Hata uki.uangalia saiv anapiga kazi sana kumzidi marcelo
 
Pamoja na kutwaa mataji yote ya england na kufika robo fainali ya UEFA bado hakuna mchezaji yeyote wa city kwenye kikosi bora cha dunia. Imagine hata benardo hayupo. Cha ajabu unakutana na wachezaji 4 wa Real madrid, timu ambayo haikuwa na msimu mzuri.

Mfano mtu kama marcelo alikuwa anapigwa benchi na kale ka regulion lakini yupo kwenye kikosi. Pia mtu kama mane kaupiga sana msimu uliopita lakini hayupo.

Mtazamo wangu kikosi kilichotangawa hakiakisi uhalisia kabisaView attachment 1214670
Siasa zimeingia hadi ulimwengu wa soka, ni mwendo mdundo tu wa mbeleko mbeleko [emoji23]
 
Hakuna maana yoyote wapiga kura wanawapigia wachezaji wanao wapenda bila kujali wanafanya nini, tusije kushangaa Dan Alves anarudi tena kwenye Fifa pro XI 2020
 
Tatizo city wanamuona KDB na msimu ulioisha alikuwa majeruhi kukosekana kwa benardo silva hapo ni aibu
 
Hakuna maana yoyote wapiga kura wanawapigia wachezaji wanao wapenda bila kujali wanafanya nini, tusije kushangaa Dan Alves anarudi tena kwenye Fifa pro XI 2020
Nadhani FIFA pro xi huandaliwa na jopo la wataalamu wa FIFA na sio kwa kura tofauti na tuzo zenyewe au?
 
Jopo la wataamu wa football hawana control wala vigezo ndio maana wanamchagua Marcelo wakati team yake msimu mzima kawekwa benchi, hakuna wataalamu kwenye uchaguzi wa ubora wa wachezaji,mapenzi kwanza mengine badae
 
Wamebugi ile mbaya.Wangemweka robertson na Trent.
 
Pamoja na kutwaa mataji yote ya england na kufika robo fainali ya UEFA bado hakuna mchezaji yeyote wa city kwenye kikosi bora cha dunia. Imagine hata benardo hayupo. Cha ajabu unakutana na wachezaji 4 wa Real madrid, timu ambayo haikuwa na msimu mzuri.

Mfano mtu kama marcelo alikuwa anapigwa benchi na kale ka regulion lakini yupo kwenye kikosi. Pia mtu kama mane kaupiga sana msimu uliopita lakini hayupo.

Mtazamo wangu kikosi kilichotangawa hakiakisi uhalisia kabisaView attachment 1214670
hicho kikosi cha FIFA kikicheza na MAN CITY ya pep kinapigwa ata 5 bila majibu
 
Watu mnazunguka weee! Mnashindwa kusema ukweli kwamba nafasi ya Ronaldo alistahiri MANE nafasi ya Mbappe alistahiri B. Silver
 
Modrich, mbappe na marcelo for mane benardo na anold
 
Back
Top Bottom