Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi za Kwa Maslahi ya Taifa.
Naangalia mijadala mbalimbali ndani ya Bunge , naliona kama Bunge limedorora fulani hivi, limepoza, Mbunge pekee machachari wa CCM, Luhaga Mpina yuko nje kwa kadi nyukundu. Wakina Msukuma, Kibajaji, Dr. Kingwagala wapo kama wapo wapo tuu!.
Japo mimi ni kada wa Chama cha Mapinduzi CCM, ni wale makada wa CCM contemporary ambao kwetu ni maslahi ya taifa mbele, ndipo tuje kwenye maslahi ya chama, Bunge hili ni Bunge la CCM and CCM only!, hivyo kukosekana kwa kambi ya Upinzani Bungeni ni janga kubwa kwa mustakabali mwema wa siasa za nchi yetu.
Hivyo baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2020 tulishauri Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni? , sasa hiki kilichotokea uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020 kinakwenda kutokea tena uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025. Je nini kifanyike?.
Tena kuna wengi walishangazwa na matokeo ya uchaguzi wa 2020 hadi Chadema kuuita ni uchafuzi na kuamua kususa, lakini akina sisi hilo tuliliona toka ile ile 2015 na tukasema humu Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020? tukasema tena Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja? na tena The Economist: Rais Magufuli ametangaza kufuta Upinzani ifikapo 2020 na kuirudisha Tanzania kuwa Nchi ya chama Kimoja na tena
Pengo la kukosekana kwa wabunge mahiri kama Zitto Kabwe, John Mnyika au wabunge machachari kama Tundu Lissu, linaonekana wazi kwa mijadala iliyodorora, na kukosa msisimko!. Angalau kidogo session ya jana ya kipindi cha maswali ya papo kwa papo na Waziri Mkuu, wapinzani walipewa nafasi waka amsha amsha. Kina Halima Mdee, Esta Bulaya, Esta Matiko na wapinzani wengine ukimuondoa ni kama wamemwagiwa maji na kujikunyata huku wamepoa kabisa zile cheche zao za Bunge lililopita.
Nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili kutokana na hoja za mwana jf huyu
Hivyo nilimuombea Tundu Lissu ate uliwahi ubunge kwa yule Blaza wangu For the sake of National Unity, Je tumshauri Dkt. Magufuli aahidi kumteua Tundu Lissu kuwa Mbunge?
Hivyo uchaguzi wa 2025, kama CCM itamsimamisha Samia, then Samia ndie mshindi wa uchaguzi wa 2025 hivyo kwanza nimeshauri wapinzani Kuelekea 2025 - Kama Upinzani unataka mafaniko ya kweli 2025, Iachane na Urais, Ujikite Serikali za Mitaa, Ubunge na Udiwani, Urais labda 2030!
Pili nikashauri Iwapo Watanzania wataamua 2025 twende na Mwanamke, mnaonaje tukiwashauri CHADEMA wasimamishe Mwanamke? Maana Mwanaume kushindwa na Mwanamke ni aibu!
Kwa hali ya siasa zetu ilivyo mpaka sasa hapa tulipo, kwenye the politics of hostilities and confrontations, kilichotokea uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020, kinakwenda kutokea tena uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025 ni CCM and only CCM!.
Hivyo ili Tundu Lissu na wapinzani wengine waingie Bungeni, then 2025 wasigombee urais na Samia, badala yake wagombee ubunge.
Yale mazungumzo ya maridhiano yarejelewe, watu wakae mezani wagawane nusu mkate.
Baadhi ya majimbo likiwemo jimbo lake yaingizwe kwenye ule mpango wa nusu mkate.
Na hata Tundu Lissu akigombea Urais kwa tiketi upinzani, agombee kwa ajili tuu ya kupata kura za ubunge wa viti maalum na sio kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Urais wa Tanzania na Zanzibar ni haki miliki ya chama kimoja tuu CCM!.
Hivyo Tundu Lissu akigombea urais, ataukosa, ila tutamuomba mama yake mdogo, Rais Samia, anayemuita mwanae na kwa jinsi anavyompenda hata kumbatiza yule Simba wa Kizimkazi kumuita Tundu Lissu, amteue kwenye zile nafasi zake 10 hivyo 2025, inyeshe mvua, liwake jua, afe kipa, afe beki ni Tundu Lissu na wapinzani wengine Bungeni!.
Bunge la 2025 liwe na msisimko kwasababu Bunge hili kiukweli ni kama limedorora fulani hivi kutokana na kukosekana kwa wabunge machachari kama Tundu Lissu, Zitto Kabwe, John Mnyika, Heche, Sugu and the like, Je mazungumzo ya maridhiano yaendelee ule utaratibu wa kugawa nusu mkate utumike kuwarejesha wapinzani Bungeni ile 2025 akiwemo Lissu au kuliko kuwa wabunge wa hisani ya nusu mkate, bora wapinzani wakomae kwa kupambana na hali zao, watatusua tuu hiyo 2025, na kuwa wabunge wa kifua mbele na sio wabunge wa hisani?
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali

Kwanza naunga mkono hoja TL aingie Bungeni, ule uchaguzi wa 2020, japo mimi ni miongoni mwa watu tuliomchagiza kugombea urais Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli! lengo ni ili tuu kuutia joto Urais mtu asiupate kwa ulaini kama anakwenda msalani, lakini mimi ni realist najua urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania una hakimiki ya chama kimoja tuu, chama dola CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola![*]Tundu Lissu: huyu kiongozi hatakiwi kukosa kabisa bungeni. Kama chama kingeruhusu huyu kiongozi angegombea nafasi ya urais na ubunge kwa pamoja. Tundu Lissu ndie kiongozi pekee kwa upinzani anaweza kupambana na kiongozi yeyote wa CCM ngazi ya urais na yeye akaibuka mshindi. Lakini endapo atahujumiwa kwenye nafasi ya urais tusimkose kwenye bunge la 2025- 2030 atatusaidia sana kuzuia sheria mbovu na Madudu mengi.