Kuku ana matatizo

Kuku ana matatizo

chayowa

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2011
Posts
413
Reaction score
110
Habari wajasiriamali..... mimi Ni mfugaji ninayejifunza kuwa mfugaji bora... kuna kuku nimemkuta anatoa machozi na anavitu vyeupe machoni... nimejaribu kumsafisha na maji ya vuguvugu na chumvi kama huduma ya kwanza.. Naomba aliyewahi kutana nao akauweza anisaidie....
 
Attachments

  • 1420264961667.jpg
    1420264961667.jpg
    57.5 KB · Views: 404
  • 1420264979941.jpg
    1420264979941.jpg
    44.2 KB · Views: 369
Lifungue hilo jicho halafu libinye kitatoka kitu cheupe kama mahindi halafu muwekee dawa ya unga IPO kwenye kichupa cha njano inaitwa RADAMYCIN .... pia ninakushauri uwawekee na kuku wengine katika banda
 
Pole mkuu, kama upo Dar beba kuku mmoja mgonjwa nenda nae farmers choice Ilala watakuambia ugonjwa na tiba .
 
KUKU WAKO WANAPATA CHAKULA GANI? NENDA KWA DAKTAR WA MIFUGO NA UYO KUKU..AU SUBIRI mama joe, chacha pountry na wengineo watakujuza.
 
Asanteni sana wadau..... bluetooth nimekupata.... ndio narudi mihangaikoni.... Ni kweli nimembinya ametoa kidude cheupe kama kiugali... kesho mapema naenda nunua hiyo kitu
 
Chuck.... nawapa sana pumba.... ila pia mara nyingine nawachanganyia mashudu, soya na dagaa
 
Mkuu choya wahi,,ukichelewa kama huyo hata ukitoa ugali jicho ni kwishna sokama macho mawili ni unachinja amakupikia mbwa wako,,wahi peleka pale ubungo oilcom gorofaya kwanza kuna dk mzuri wanakupa nadawqzqke,,polemfugaki
 
huyo/hao kuku anaweza kua anaumwa ugonjwa wa coryza maana sijaona masundosundo (nodules) ningesema ni ndui, ama pia hujasema kama anatembea au amepooza miguu na mabawa ningesema ni kideri.
ugonjwa (infectious coryza) unaenezwa kwa njia ya hewa, chakula na maji hivyo zingatia usafi katika banda na pia kuwe na mzunguko wa hewa ya kutosha.
matibabu: nenda duka la madawa ya mifugo la karibu yako kawaeleze tatizo watakupa appropriate antibiotic (dawa husika).
kila la heri
 
Naskia kuku wakiugua coryza hawatapona kabisa bali watabaki kuwa carriers, na hizi signs za coryza zitakuwa zinajirudia rudia na itahitajika wawe wanapewa hizo antibiotics kila signs zinaporudi. Hii ni kweli mkuu?
 
yap ni kweli, wanakua carriers and source of infections to un affected ones. vitu muhimu ni kutibu pale wanapoonesha signs ila muhimu zaidi ni usafi wa banda, hewa ya kutosha, lishe bora na pia epuka kuwa "stress" hao kuku. mara nyingi stress huamsha (lead to outbreak) magonjwa mengi ya kuku.
 
polesana kukuwako anaumwa ugonjwa wa upungufu wa vitamini A. hauna tiba. unakingwa kwa kuwapa majani mabichi.

ni sawa ulivozungumza lakini ni vema kujua anawalisha chakula gani na anawafuga ufugaji upi kama ni huria au wa ndani. mara nyingi upungufu wa vitamins huwakumba kuku wanaofugiwa ndani (intensive) ambapo moja ya dalili ni kutokea kwa madubwana machoni (keratinization of the third eyelid).
ila kwa hiyo case mimi sidhani kama ni avitaminosis.
 
huyo kuku amekosa vitamin c hvyo kanunue vitamalt uwape alaf tafta dawa yeny antibiotic umpe huku ukiendlea na kumsafisha...ikishindkana kanunue dawa ya macho ya binadam boric acid umuweke kila ukimsafxha....ndvyo nlvyo fany nkafanikiwa....
 
Chawoya hebu rudi hapa na feedback

Kuku wako amepata matibabu stahiki???
 
Last edited by a moderator:
Hao kuku wako wana umri ganai. Inaonekana hukuwachanja ndui itafika mda mcho yataanza kuoza. Ulitakiwa kuwachoma ndui wakiwa na miezi 3. Pia zingatia vitamin ndio nguzo ya mifugo yako
 
ni sawa ulivozungumza lakini ni vema kujua anawalisha chakula gani na anawafuga ufugaji upi kama ni huria au wa ndani. mara nyingi upungufu wa vitamins huwakumba kuku wanaofugiwa ndani (intensive) ambapo moja ya dalili ni kutokea kwa madubwana machoni (keratinization of the third eyelid).
ila kwa hiyo case mimi sidhani kama ni avitaminosis.

Nilicho kieleza ninakijua vizuri sana na nimepata semina SUA. huo no ugonjwa Wa ukosefu Wa vitamin A. nitofauti na ndui ya Kuku, ndui Kuku anakuwa na mapele kichwani na mdomoni. lakini huu uko ndani ya jicho, jicho huziba na ukilitumbua linatoa maji na kitu kama sabuni iliyo lowekwa.MTOA MADA njoo hapa ukanushe kamaniliyo andika hapa ni uongo hayatokei kwa Kuku wako.Ugonjwahuu hauna Tiba Bali unakinga
nayo ni kuwapa majani mabichi. Kuku akiugua huyo keshakuwa kipofu.
 
Hii ni raha ya kuwa jf memba yaani mtu unasaidiwa shida yako kwa kihasi kikubwa na kwa gharama nafuu sana sana.mungu awazidishie mema tele
 
Ebwana kuku nawafuga ndani... kwa hiyo yawezekana Ni ukosefu wa vitamini... ndui walipata kwa muda muafaka.. niliwasafisha na kuwaweka dawa kila asubuhi na jioni.... kwa kweli wamekuwa wanakufa na inaonekana kweli Ni carriers... Sasa nawaeka dawa ya macho ya binadamu na mchicha kwa wingi... sijaona tatizo karibuni....
 
Back
Top Bottom