Je, una mtaji wa kutosha?!
Kama una mtaji wa kutosha basi fuga kuku wa mayai! Mbegu za siku hizi ni bora sana kiasi kwamba, ukifuata kanuni bora za ufugaji basi kila siku utaokota mayai hadi 90% ya idadi ya kuku wako!
Hii maana yake ni kwamba, ukiwa na kuku 1000, basi kwa siku unaweza kupata mayai 900 ambazo ni trey 30.
Ninaposema kanuni bora za ufugaji ni pamoja na banda ya kisasa lenye ventilation ya kutosha na hivyo kuwawezesha kuku kupata hewa ya kutosha, and in turn, kutokuwa wavivu wa kula! Kuku akila vizuri ina-guarantee utagaji mzuri!!
Ninaposema kanuni bora za ufugaji pia tunaangalia utolewaji wa chanjo at the right time!! Ukishajenga tu banda, kabla hujaweka kuku, onana na mtaalamu wa mifugo akushauri!!!
Ninaposema kanuni bora za ufugaji ni pamoja na kutowabania chakula! Kuku anayepunjwa chakula hawezi kutaga vizuri lakini kwa bahati mbaya sana, chakula cha kununua ni very expensive, ndo sababu ya watu kuwabania kuku chakula bila kujua utakuwa unawabania kutaga vile vile!!
Kwavile chakula ni very expensive, unashauriwa kutengeneza mwenyewe kwa kutumia formular maalumu, na sio kuchanganya changanya tu hovyo hovyo!!!
NInaposema kanuni bora za ufugaji ni pamoja na kuhakikisha banda linakuwa safi and free from majimaji! Banda chafu na lenye maji maji ni chanzo cha magonjwa kwa kuku!!
Ninaposema kanuni bora za ufugaji, ni pamoja na kuweka kitu cha kupangusia miguu kwenye mlango wa banda ili kuhakikisha hutoi vijidudu huko nje na kuingia navyo bandani! Hakikisha hiki kifutio kinakuwa disinfected regularly!
REMEMBER, kuku anaweza kutaga kwa miaka 2 (miezi 24) however, wakishafikisha miezi 18 rate ya mayai itakuwa ina-drop! Best economic practice ni kufikiria kuwasimamisha ikishafika miezi 18 hata kama bado wanataga UNLESS ujiridhishe idadi ya mayai wanayotaga inakupa pesa ya kutosha kuweza ku-cover costs zote, na wewe kubaki na faida!
REMEMBER, bei kubwa ya vifaranga utakuja ku-compansate kwa kuuza hawa kuku unaowaachisha kutaga!!
Katika hali ya kawaida, kila siku utakuwa unaingiza almost 50% ya total variable costs, na kama chakula unatengeneza mwenyewe, basi utakuwa unaingiza over 50%!
REMEMBER, kuku wa mayai unawahudumia angalau miezi 5 bila kuingiza hata senti 5... yaani ni kukuchomoa tu!
That being said, make sure una mtaji wa kutosha, and to be safe, weka kiasi pembeni ambacho hicho kitakuwa kwa ajili ya kuhudumia kuku tu... especially chakula!!!
Usipofuata ushauri huo hapo juu, kuna hatari itafika siku au hata wiki huna pesa na kuku wanahitaji kula! Matokeo yake, utaanza kuwabania msosi!!!
Kwa maana nyingine, kama huna mtaji wa kutosha basi anza na kuku wa nyama lakini pia hakikisha unafuata kanuni hizo hapo juu kwa sababu na washikaji na wenyewe wanakula balaa!!!
HOWEVER, make sure unapata uhakika wa soko kwamba na usipofanya hivyo, utalazimika kuendelea kuwalisha wakati walitakiwa tayari wawe sokoni, na hivyo kukuongezea gharama zisizo na msingi, and in turn loss or faida kiduchu!
Kuku wa Kienyeji sikushauri unless kama unataka kufanya Free Range; ufugaji ambao sio mzuri kibiashara!!!