Bwana sikia ndugu yangu usitake mbwembwe usitake pesa za haraka,Ndio kila mtu anahitaji pesa ila ki ufupi mpaka sasa sijaona ufugaji ambao una pesa tena pesa kweli kweli kama ufugaji wa kuku wa kienyeji.
Kuku wa mayai kila mtu anafuga,mnakutana kwa Mangi kila mtu na mitrei yake kibao hamjui wakumuuzia,Kuku wa nyama kila mtu anafuga imefika hatua kuku mzima anauzwa 4000 (hiii ni nini eti) tusifate mkumbo kwenye ufugaji SOKO litakua gumu na hivi makuku yenyewe ya kisasa,mayai yenyewe ya kisasa (stress tupu).
Hela ya kweli wajuba wanakwambia REAL MONEY imejificha kwenye mabawa ya kuku wa kienyeji,kuku wa kienyeji ni pesa Ni gold inayotembea,Ujue namna ya kumfuga/kumlea hadi kupata product tamu.
Haya ni mawazo yangu na ushauri wangu,kama kweli unataka pesa isiyo na stress kwa kiasi kikubwa basi ufugaji pekee wa ki don wa ki pofa ni wa kuku wa kienyeji.
Tafuta mfanyabiashara/Mfugaji wakuku wa kienyeji alie karibu yako akumegee siri usizojua,usiende omba ushauri wa kufuga kuku wa kienyeji kwa mfuga broiler au kuku wa mayai.