Kuku huyu ananishangaza!

Kuku huyu ananishangaza!

Mama Joe hivyo virutubisho ni aina gani?
na ikiwa kuku wa kienyeji anafugwa tu kwenye banda inapaswa ale nini?
Tuliongelea sana kuhusu chakula na madawa kwenye uzi wa Kubota wa "zijue mbinu zangu..." anu pitia uzi wa Amani Ng'oma "kwa wanaotaka kuanzisha ufugaji..." hata yeye anajibu maswali ni mtaalamu. Kifupi kuku wadogo wa siku moja hadi miezi 2 wanakula starter, na kuanzia hapo kuna Layers finisher. Tatizo wanaotayarisha vyakula mara nyingine wanalipua au kuku wenyewe wakiwa aidha wanataga inabidi uongeze virutubisho. Kuna mifupa, kuna DCP, endapo unaweza waweza kuwapa vitamin kila unapowapa chanjo mfano Newcastle kila miezi mitatu au unapoona utagi mdogo au mayai yako weak. Vinginevyo kama ni majogoo tu wapo fit hiyo finisher kama ni quality inatosha kabisa. Kwa wale wanaofugwa ndani bila kutoka nje kula wadudu na majani itabidi uwape majani na ukiweza wengine huwatengenezea minyoo wamefundisha kwenye maada zote mbili hapo juu. Hawa hata mabaki ya chakula unawapa ila view havijaharibika na wawekee kwenye vyombo sio chini. Kupunguza gharama unaweza kununua concentrates ukaichanganya kwenye pumba na kupata finisher.
 
Back
Top Bottom