Kuku kuchi hawa ni original?

Bado sijaona sababu yenye mashiko kuuzwa bei kubwa hivyo.
Haya mapo yanakujaga kama network marketing tu ukiyafatilia hakuna uhalisia.
 
Hao kuku ni wenyewe, wazuri, naweza kusema haujapigwa (ila inategemea na bei uliotoa).

Bei zao hua kuanzia 100,000/= mpaka 300,000/=. Nliwahi kufuga kuchi zamani kidogo.
Nashukuru sana kiongozi nimewanunua kwa moyo mmoja kabisa sababu tulio nunua hiyo siku tulikua watatu na waligombaniwa sana ila nimekuja huku kwa wadau kujidhiirisha na kupata uhakika zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukimnunua laki moja alafu ukapata mteja wa wa laki mbili ndo utashawishika kaka kama nilivyoshawishika mimi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo mambo yapo kama network marketing. Ukitaka kuamini shangaa hata ww hujui sababu za msingi kuuzwa bei kubwa.
Chukulia mfano hawa wa tuliowazoea ndio wangekuwa tunafuga kama hao bei ingeporomoko ushangae.
Sasa wewe jiulize wanatumika kwa kazi gani?
 
Jamaa mmoja kasema wanapiganisha kwenye kamali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tupe mwongozo uliishia wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
Masomo, ilibidi nisafiri kwenda mbali kwaajili ya masomo halafu sikua na mtu wa kuwaangalia. Ikabidi niuze wote. Ila ukituliza kichwa hao kuku watakutoa kimaisha, utapiga hatua sana. Utakua haukosi 300,000/= au 200,000/= za haraka haraka.

Sema jitahidi uwe unawapa kinga kila baada ya miezi mitatu, magonjwa yanaosumbua kuku hua ni Sotoka, Gumboro na Mafua (Na yote yana kinga zinauzwa madukani) kuna magonjwa mengine kama minyoo sio hatari sanaaa hua wanapona. Ukiweza kuwapa kinga za hayo magonjwa matatu kila baada ya miezi mitatu basi mambo yatakua poa sana.
 
Mbegu zake zinauzwa wapi????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…