kuku kuchi

faiz jr

Member
Joined
Aug 18, 2013
Posts
31
Reaction score
3
nina kuku kuchi wadogo wana miezi kama miwili ila ukuaji wao ni wa taratibu sana,kwa yeyote mwenye uzoefu nao naomba aniambie ndo kawaida yao kukua taratibu au hawa wangu wana matatizo?
 
Ndivyo walivyo na hata Jogoo la kuchi likianza kuwika utashangaa anaanza akiwa mdogo ila kwa uzito tu nawasifu utakiona kidogo lakini kibebe uone
 
je makoo wanaanza kutaga wakifikia miezi mingap? kuna mtu aliniambia wanaweza kufika miezi 10 ndo wanaanza kutaga,je ni kweli?
 
je makoo wanaanza kutaga wakifikia miezi mingap? kuna mtu aliniambia wanaweza kufika miezi 10 ndo wanaanza kutaga,je ni kweli?

Sio kweli mimi nawafuga sana wastani wa kuku ambaye hana matunzo kutaga kwake huanzia miezi sita hadi saba, huyo aliyekuambia miezi kumi anakukstisha tamaa
 
asante kwa msaada wako,je wewe unao kuchi? na bei zake zipoje?
 
asante kwa msaada wako,je wewe unao kuchi? na bei zake zipoje?

Bei ya soko sasa hivi sijapata uhakika wa bei maana hua na bei tofauti tofauti,, Na vile vile mie ninawafuga wa kuendeleza kizazi sio kwa kuuza!!
 
Bei ya soko sasa hivi sijapata uhakika wa bei maana hua na bei tofauti tofauti,, Na vile vile mie ninawafuga wa kuendeleza kizazi sio kwa kuuza!!

unapatikana wapi nije kuwaona? niwafananishe na wangu,tubadilishane mbinu za ufugaji wao?
 
Mkuu, mimi nipo katika mchakato wa kuanza kufuga kuku na sasa naandaa shamba huko Kibiti. Ajabu nimeenda huko nkakuta kuku wana maumbile madogo ingawa wenyeji wanasema hao ndo kuchi, nkashangaa kweli ila naambiwa ni wazito. Mimi nijuavyo kuchi huwa ni mkubwa na manyoya kidogo. Jaman naomba kujuzwa zaidi.
 
kuchi ni wakubwa sana akiwa mkubwa mpaka 2.5kg...wakorofi..waukweli ni znz mkubwa mpaka laki
 
kuchi ni wakubwa warefu wana miguu mirefu,hao ulioneshwa inawezekana ikawa sio kuchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…