- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
- Tunachokijua
- Madai
Kumekuwapo kwa Kipande cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii inayomuonesha miongoni mwa kuku waliokufa akitoa moto mdomoni kila akikandamizwa na mtu anayeonekana kumshika. Taarifa hizo zinaeleza kuwa tukio hilo limetokea nchini India. Tazama hapa na hapa
Uhalisia wa video hiyo
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa video hiyo imeanza kusambaa katika mitandao ya kijamii kuanzia Disemba, 2024. Tovuti mbalimbali zilieleripoti kuhusu tuko hilo kuanzia tarehe 27 Diemba 2024.
Tovuti ya Hindustan Times walichapisha taarifa wakieleza kuwa Kijiji kimoja huko Karnataka kilishuhudia tukio la ajabu ambapo kuku 12 walikufa katika mazingira ya kutatanisha na kuanza kutoa miale ya moto kutoka midomoni mwao wakati miili yao ilipokandamizwa. Video iliyosambaa mtandaoni inaonyesha kuku hao wakiwa wamekufa wakilala chini, huku moshi ukipanda kutoka miili yao. Wameeleza pia chanzo kimoja kiliripoti kuwa mmiliki wa kuku hao, Ravi alisema kuwa ameripoti kwa mamlaka wachunguze kuhusu tukio hilo. Tovuti nyingine zimehifadhiwa hapa na hapa
Licha ya kudaiwa kuwa taarifa hiyo imeripotiwa kwa mamlaka kwa ajili ya uchunguzi lakini hakuna mahali ambapo wameandika kuhusu majibu ya uchunguzi huo. Hakuna uthibitsho pia wa moja kwa moja iwapo tukio hilo linaweza kutokea kwenye hali ya kawaida.
Ufuatiliaji kupitia nyenzo ya Hive moderation imeonesha kuwa asilimia 95 ya video hiyo inaweza kuwa imetengenezwa kwa akili mnemba.