Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inawezekana,kinachotakiwa ni matunzo na chakula bora unaweza ukakiandaa mwenyewe kinakua bora zaidi,pia kuwapatia chanjo za magonjwa hatarishi.
mkuu unaweza kunipa dondoo za uandaaji chakula cha kuku bora. Wakitaga kama wa mayai wanatoa asilimia ngapi?
Nenda ukagogle ufugaji kuku wa kienyeji,utakuta kuna pamflet moja imeandaliwa na mradi ...nimesahau jina ila kwa msaada wa Swiss Aid for rural Development utapata kila kitu.mimi mwenyewe nilisoma humuhumu na sasa nina kuku wa kienyeji 250 nategemea mwishoni mwa mwezi huu wataanza kutaga.
Hapo kwenye kutoa asilimia sijakuelewa,kuhusu uandaaji wa chakula nitakuandikia usijali.
Mtakuwa mnazungumzia Chotara, Ila pure Kienyeji haiwezekani wakawa wanataga kila siku ni lazima wafikie mahali wanastop kwa ajili ya kuatamia, hivyo mambo ya kutaga kila siku ni hakuna hata kama utawapatia chakula cha aina gani,
sawa ila kumbuka wa kienyeji baada ya mayai kama 12 ni lazima atake kulalia na kumsahaulisha huchukua si chini ya wiki mbili hadi tatu kuanza kutaga tena.lakini hata kuku wa kisasa kutaga kila siku haiwezekani maana mzunguko ukifika mwisho lazima atastop ndo aanze tena ndio maana hata ukiwa na kuku 100 wa mayai huwezi okota mayai 100 kwa siku
sawa ila kumbuka wa kienyeji baada ya mayai kama 12 ni lazima atake kulalia na kumsahaulisha huchukua si chini ya wiki mbili hadi tatu kuanza kutaga tena.
mpaka sasa sijapata changamoto yoyote ambayo ni kubwa ,mm vifaranga nilinunua kutoka kwa kampununi moja inaitwa BenaChicks wako mbagala,walinipa karatasi inayoonyesha maelekezo yote ya utunzaji(kwa maana ya chanjo, na chakula na nimefuatilia maelekezo sijaona shida yoyote) kwa wastani ktk kuku mia vilikufa vifaranga 2.kwa sasa wanamiezi 3 na 2weeks.majogoo yameshaanza kuwika na yana wastani wa 2kg.
Kwa alieuliza kuhusu ratio ya chakula unafanya pumba ya mahindi kg 30,mashudu ya alizeti kg 20,uwele/mtama kg20,pumba ya mchele kg20;dagaa wachafu kg5,mifupa kg5,chokaa kg 1(sio lazima),chumvi pakiti moja hiyo ni kwa kilo mia.
nimefurahia mchanganyiko huu, natumai unakupa tija kwenye ufugaji wako.
Naomba niuchukue kama ulivyo nami uninufaishe, ila sijaelewa kwanini unatumia mifupa na chokaa wakati mmoja.
Shukran.