Kuku wa kienyeji:msaada please

Kuku wa kienyeji:msaada please

NGARUKA

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
401
Reaction score
70
nina mambo nataka kusaidiwa kuhusu ufugaji wa kuku wa kienyeji.
1.Kuku wangu wanataga mahali pamoja,je hawatanisumbua wakitaka kuatamia?
2.Nipeni uwiano wa Majogoo wangapi kwa majike,alafu mbona majogoo yanafukuzana tu na mzigo hayapigi?
3.Naombeni mnifhamishe dawa angalau ambayo ni "general purpose" kwa magonjwa ya kuku.
Jamani mi ndo naanza ufugaji nielekezeni.
MUBARIKIWE WANA JF
 
search search hapa kuna topics zilizopita ambazo utajifunza mengi
 
Apolinary nashukuru sana ngoja niwaache tu hivyo. Vp kuhusu dawa za kuku
 
Mkuu kama unawafungia Ndani Uwiano unao takiwa ni 1:10 hii haina shida kabisa ila kama wako huria inatakiwa iwe 1:6 hii inasababishwa na ile kufukuza fukuza sana jogoo anachoka hivyo ukiweka majogoo wachache halafu mitetea wengi ndo utakuta mayai mengi yanakuwa ni unfertilized yaani hayana mbegu kabisa.

DAWA ZA HUDUMA YA KWANZA AMBAZO HUTAKIWI KUZIKOSA NI

1. OTC 20

2.Esb3

3. Amprolium

4. Vitalyte/Amylite

Hizo ndo za huduma ya kwanza ingawa wadau wataongezea zingine nyingi tu
 
Nashukuru Chasha. Upande wa uwiano nimekuelewa kabisa. sasa hizi dawa ni aidha upate zote au mojawapo.
Nisaidie na dawa ya kuondoa utitiri.
Wabheja sana
 
Dawa ya utitiri zipo za unga kama Akheri Powder, severin n.k. Ama waweza tumia ya kunywa, Kepromec hii ni ya minyoo pia inasaidia utitiri na wadudu wengi kwenye ngozi

Kila la heri mkuu
 
nashukuru RETI umenisaidia sasa naweza tatua matatizo mwenyewe.
Mbaraikiwe sana
 
Mkuu kama unawafungia Ndani Uwiano unao takiwa ni 1:10 hii haina shida kabisa ila kama wako huria inatakiwa iwe 1:6 hii inasababishwa na ile kufukuza fukuza sana jogoo anachoka hivyo ukiweka majogoo wachache halafu mitetea wengi ndo utakuta mayai mengi yanakuwa ni unfertilized yaani hayana mbegu kabisa.

DAWA ZA HUDUMA YA KWANZA AMBAZO HUTAKIWI KUZIKOSA NI

1. OTC 20

2.Esb3

3. Amprolium

4. Vitalyte/Amylite

Hizo ndo za huduma ya kwanza ingawa wadau wataongezea zingine nyingi tu

Mkuu tafadhali unaweza kutusaidia kuweka maelezo kila dawa hapo ni kwa ajili ya nini/ugonjwa gani! Asante
 
OTC 20- Hii inatibu magonjwa mengi na ni moja ya dawa nzuri sana kwa ajili ya huduma ya kwanza(OXYTETRACYCLINE AU SALFA)
-Hutibu Homa ya matumbo
-Hata kwa mafua ya kuku ni nzuri pia kwa sababu ina salfa
coccidiosis

Esb3- Hii ni kwa kipindi pindu ile ya kuhara chokaa

-Amprolium- Hii inatibu Coccidiosi na pia ni kinga kwa huo huo ugonjwa yaani wanaweza pewa bila hata kuumwa

-vilyte- sio dawa bali ni vitamini tu kwa ajili ya kuwapa kuku
-
 
-[/QUOTE
Asante mkuu na huwa wanapewa dawa hizi kipindi gani? Chanjo au wakiugua?
 
OTC 20- Hii inatibu magonjwa mengi na ni moja ya dawa nzuri sana kwa ajili ya huduma ya kwanza(OXYTETRACYCLINE AU SALFA)
-Hutibu Homa ya matumbo
-Hata kwa mafua ya kuku ni nzuri pia kwa sababu ina salfa
coccidiosis

Esb3- Hii ni kwa kipindi pindu ile ya kuhara chokaa

-Amprolium- Hii inatibu Coccidiosi na pia ni kinga kwa huo huo ugonjwa yaani wanaweza pewa bila hata kuumwa

-vilyte- sio dawa bali ni vitamini tu kwa ajili ya kuwapa kuku
-

Be blessed Chasha
 
Last edited by a moderator:
dawa ya vifaranga kupinda miguu na kutembelea magoti. Nisaidien
 
Mkuu chacha naomba unisaidie yafuatayo...
- gumburo ni ugonjwa gani?
- naomba unipitie ratiba ya kuwapa chanjo kuku kuanzia anapototolewa... Kuanzia wiki ya kwanza...
- ni lazima kuwakata kuku midomo
Asante mkuu
 
1. OTC 20

2.Esb3

3. Amprolium

4. Vitalyte/Amylite

Hizo ndo za huduma ya kwanza ingawa wadau wataongezea zingine nyingi tu

Mkuu hebu nisaidie kujua hiyo namba 4 inatakiwa kutolewa kwa kuku (wa kienyeji) kila baada ya muda gani?
 
Back
Top Bottom