Kuku wa kienyeji

Kuku wa kienyeji

Brown73

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2010
Posts
1,100
Reaction score
682
Habari za kazi ndugu wana JF.
Nimejaribu kufuga kuku wa kienyeji na machotara huko vijijini sehemu za tanga, kwa majaribio hayo nime anza na wachache sana kama 250 wa umri tofauti, sasa wamesha kua wakubwa tatizo ni soko. Lengo langu ilikua niwe na kuku 1000 kwa mwezi.
Nili jaribu kosoma articles humu ndani ya JF wengi wakisema kua kuna biashara nzuri na wana bei nzuri ingawa ni nyuzi za zamani zilizo andikwa humu. Je wama jamvi kuna mtu au watu wanao fahamu kuhusu biashara hii hapo dar es salaam au tanga, kama kuna soko zuri na bei nzuri. Kwa hapo kijijini wanataka 7000 kwa jogoo mwenye miezi minne na nusu na hiyo bei ni ya hasara kabisa, ni sawa na bei ya broilers.
Kama kuna mtu anafahamu kuhusu biashara hii tujaribu kuwasialina, niko tiari ku invest na kufuga kwa kusupply hata zaidi ya kuku 1000 kwa mwezi, mradi soko la uhakika tu na bei nzuri.
Ahsanteni.
 
ndugu yangu
hongera saana
Soko la KUKU wa KIENYEJI
halijawahi kuwa tatizo

.......nakushauri......
kabla hujaja Dar es salaam, ni vema ukaanzia hapo ulipo kwanza
hapo ulipo..kuna mahoteli na watu binafsi pia..ungeanza nao ingekuwa njia rahisi saana ya wewe kupata uzoefu..sasa DSM ukipewa soko ukaambia kila wiki uwe una supply kuku 300 bila kukosa utaweza?????
 
Nashukuru sana kwa jibu lako ndugu Prodigal son.

Hilo ndio ilikua wazo langu kabisa, nianze kwanza hapa nilipo ili kupata uzoefu, sasa nikisha anza kupata connection za DSM au mtu wa kushirikiana nae huko DSM basi nizidishe uzalishaji, Sasa nimeacha mitetea kama 80 hivi ambao nategemea wawe parents, watage ni nitotoe vifanranga mwenyewe kama nitapata incubator nzuri au niwaachie hao kuku wenyewe waangue vifaranga then niwanyanganye wakiwa na wiki mmoja. Biashara muda mwingine huwezi ukafanya mtu mmoja inabidi ushirikiano kidogo na pawe na uaminifu.
kilicho nishtua tu leo ni hiyo bei waliotaka kwa 7000 kwa jogoo ukizingatia kuku umemlisha na kumtunza zaidi ya miezi minne
 
Hako ni kachangamoto kadogo sana, ungesema watu hawataki kununua kuku wako ningekuna kichwa !!!!!. Jipange vizuri kuhusu uzalishaji, soko la Dar linataka kuku wengi sana, tatizo ukishapeleka trip tatu hivi unaishiwa mzigo. Mimi ningekushauri pia kuangalia upande wa mayai nayo.
 
Nashukuru sana ndugu malila, wazo zuri.
Niko njiani na hili la mayai.
Je unafahamu bei ya jumla wa hao kuku hapo dar? na mayai pia? kama nilivyo sema nimeanzisha huo mradu kama majaribio, Investment ya hela si tatizo ni kwamba tu huwezi fanya biashara bila ya kufanya uchunguzi na pia kupata ushirikiano.
Nashukuru sana kwa mawazo yenu.
 
Mkuu kuhusu masoko kweli kuna Changamoto, ILa hawa ndege nao wanataka Timin some timemano wakati sikukuu za idi utauza tu, na waati wa kristmas,
So kama unaona bei hailipi unaweza kuja na optional nyingi, kama vile Kuuza kwa hiyo bei ambayo ni hasara, Kutafuta watu wa kuwasambazia kwa Tanga, Korogwe na kazalika,

Mwisho unaeza kuwa the consumer of your own prduct, hapa ni kwamba kama Uko Mjini unaweza na wewe kufungua mgahawa wako na ukajikita kwenye Kuku Choma, rost na supu, so hapo utakuwa unatoa shambani na kuja kuuza mwenyewe kwa kuwachinja.

AU unaweza kuwa na Butcher ya Kuku, unawachinja na unakuwa unauza vipande vipade au nusu au Robo au mzima, so unapo kuwa na Butcher ukauza wakibakia unapeleka kwenye mgahawa wako ambao n maalumu kwa kuku tu
 
Yes, that is good idea ya kuchinja na labda ku pack na kusambaza, Lakini kufungua mgahawa labda ni mtafute mtu mwaminifu nimfungulie huo mgahawa maana mimi nimeajiriw, Infact nafanya kazi nje ya nchi ndio nafikiria kurudi home, sasa shamba ninalo panahitajika tu shughuli za kufanya, mmoja wapo ndio hiyo ya mifugo.
Hivi Chasha sio wewe anaye uza vifaranga vya kenbro?
 
Back
Top Bottom