Kuku wa kisasa

Kuku wa kisasa

jashmoe32

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2012
Posts
1,089
Reaction score
424
Habari wanajamii wenzangu,
Samahani kwa usumbufu ntakaouleta ila muda mwingi nawaza biashara gani ya kufanya na bado naona kichwa kinantesa na nimeona bora niombe msaada wa kujuzwa kuhusu kufuga kuku wa kisasa kwa ajili ya kibiashara zaidi na nlikua naomba msaada wa kujua bei ya Kifaranga kimoja cha kuku na mpaka anakua anachukua muda gani na je gharama ya kifaranga mmoja kumlisha kwa siku ni shillingi ngap?
Nlikua naulizia kuhusu sindano ya kinga wanayochomwa Kuku,je inakinga dhidi ya magonjwa yale yaliokua yanawasumbua kama kawaida au?mana kuna kipindi kuku walikua wanaanguka ovyo yani kama wanakua na ugonjwa wa kusinzia sinzia,je hii kinga ni dhidi ya huu ugonjwa au?mana kuna kipindi tulikua na Kuku 5 nao wakafa kwa ugonjwa huu wa kusinzia sinzia.

Ntashukuru nikihabarishwa zaidi mana naamini sehemu moja wapo ya kupata elimu ya maisha ni jamii forum.

Jashmoe
 
fungua uzi wa kuku wa kisasa jukwa hili hili kuna kila kitu
 
ahsante Mama Joe na nimeshausoma na nliwasliana na kampuni 1 na wakasema wanauza layers kwa 2400 na broilers kwa 1400 na nlikua naulizia je gharam ya kuwalisha layers 100 kwa mwezi inaweza ikawa sh ngap yan ukijumlisha na chanjo?
 
Ninachojua ni kuku 200 wanakula mifuko 10 hadi wiki ya 6 tayari kuuzwa. Ukikosa soko wanaendelea kula...hata mfuko kg 50 mmoja kwa siku. Wiki ya 1-4 starter 4. Wiki 5-6 finisher 6. Ni makisio kwa uzoefu lakini angalia vyombo visimwage chakula ovyo. Fanya makisio kwa kuku 100.
 
Back
Top Bottom