Kuku wa kuchoma au wakuokwa

Kuku wa kuchoma au wakuokwa

Hahahahahaha lol!!!! Chezeya mimi weye!!!! shurti gudulia la maji mezani liwepo lol! 🙂🙂🙂

Maji kwenye gudulia nimecheka mpaka nataka kupaliwa.....mie mroho huyo nala na salad tu lol
 
Mie kwenye msosi huwa sijivungi banaaaa kama ni msosi mtamu basi lazima niende nao sambamba lol!!!! Pili pili ya farkhina poa sana hata kwenye msosi huu iko bomba sana.

nishakuweke pilipili hapo BAK,au ukibadilishia na ile pilipili ya maembe ya farkhina naona utamaliza kuku mzima peke yako....
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahaha lol!!!! mmenichekesha sana farkhina na Gorgeusmimi pamoja na ubavu wa kula, kuku mzima mhhhhhh!!!!! lol!!!!! 🙂🙂 Kuvimbiwa mtindo mmoja!!!!

he he he....hafi akitoka hapo lazima ajinyooshe kwa kuvimbiwa...
 
Last edited by a moderator:
Maji kwenye gudulia nimecheka mpaka nataka kupaliwa.....mie mroho huyo nala na salad tu lol
na salad kuku mzima umle wewe :smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big:
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hahahahahaha lol!!!! mmenichekesha sana farkhina na Gorgeusmimi pamoja na ubavu wa kula, kuku mzima mhhhhhh!!!!! lol!!!!! 🙂🙂 Kuvimbiwa mtindo mmoja!!!!

Na kusinzia je maana shibe yakevya
 
Last edited by a moderator:
Kusinzia ndo nini 🙂🙂 Hapana banaaa mie hizo za kusinzia sinazo lol!!!! labda kama usiku uliopita nilikuwa najirusha kwa raha zangu kuruka debe.



Na kusinzia je maana shibe yakevya
 
Last edited by a moderator:
Jinsi ya kumatayarisha kuku
  • Mgawe kuku kwenye kifua,Mgeuze ili mgongo uwe juu na mchanechane kwenye mapaja na kifua,dhumuni la kufanya hivo ni ili viungo vikolee vizuri.
View attachment 164861
  • Kama unavyoona pembeni kuna vitunguu swaumu,vitwange na umpake mkuku,fanya kama unamfanyia masaji,weka viungo kwenye sehemu zote ulizomkata mkata hakikisha vinainga ndani,kisha muweke All around spices,na mchanganyiko wa viungo vya kuku vyenye uzile,giligilani,pilipilimanga,Kari,pilipili ya unga red paprika,endelea kumfanyia masaji tumia vidole.Malizia na juisi ya limau.Ukiwa unamuweka viungo muweke pande zote.Baada ya hapo kuku atakuwa na muonekano huu
View attachment 164863
  • Muache kuku akolee viungo masaa kadhaa.
  • Washa oven na uweke moto 200-225 degrees
  • Mchome kuku na katikati uwe unachukua ile sausi inayotoka kwa kuku na kumnyinyizia kwa juu.Akiiva juu mgeuze na upande wa pili ili apate rangi na upande huo.Mwishoni ukitaka crispy skinn weka grill juu kwa dakika tano.
View attachment 164864
  • Kuku tayari kwa kuliwa,unaweza kumla na msosi wowote,wali,chipsi ugali n.k
All around spices
View attachment 164862
Cc Revocatus Kashaga
asante sana kwa hii recipe, Mungu akubariki tunajifunza mengi sana humu
 
Dah!!! pembeni una mchicha wako wa nazi, pili pili mbuzi na ugali wa kufa mtu na gudulia la maji baridi, ukitoka hapo mpaka jasho inatoka kwa utamu wa msosi.

hahaha Yummy
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Weka mapishi ya Nzasa, niliwahi kula mchuzi wa chukuchuku na ugali kwa mnyamwezi pale kibamba baada ya kumsaidia katika shughuli za shambani kwake. Basi alikuwa analalama kwamba hana nyanya nakuomba samahani nyingi lakini mchuzi wake wa chukuchuku ulikuwa mtamu sana, sijui kwanini aliomba samahani ya kutokuwa na nyanya.

hahaha Yummy
 
Back
Top Bottom