Kuku wanakuwa walemavu!!

Kuku wanakuwa walemavu!!

Ligogoma

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2010
Posts
3,503
Reaction score
6,415
Habari wana JF,

Nafuga kuku wa mayai na wana miezi miwili sasa, tatizo limekuja kwamba wanaanza kupoteza mawasiliano baina ya viungo vyao!! Shingo inapinda na miguu inalegea yaani kiujumla wanakuwa hawawezi kufanya chochote (wanalegea) wanakuwa kama walemavu na kwa sababu wanashindwa kula huishia kufa.

Niliwapeleka kwenye maabara ya mkoa, wakasema kuku wapo vizuri sana na hawana ugojwa but inawezekana hawana vitamin lakini kiukweli nawapa vitamin ya kutosha kabisa, na kwa kufuata maelekezo na vipimo sahihi. Hata nilipowaonyesha wataalam ninavyowapimia wakabaki wanashangaa na kujiuliza tu ni nini??

Nimebaki nabuni tu labda calcium lakini nayo nimekuwa nikiwapa dawa na kuhakikisha chakula chao kina dagaa wa kutosha kabisa!! Labda hewa lakini banda lote kwa juu kwote nimeweka nyavu tu hivyo hewa ni ya kutosha kabisa.

Kwa uzoefu wenu jamani, hili linaweza kuwa ni tatizo gani??
 
pole sana mkuu ni ukosefu wa calcium, wape DCP au Di Calcium Phosphate kisha endelea kuwawekea mifupa kwenye chakula chao, umri huo wanakua na kuongezeka uzito haraka na mifupa mirefu kama ya miguu na shingoo inahitaji calcium kwa wingi ndio wanapolemaa. Hiyo maabara gani jamani, anza na DCP kisha endelea kuwaongezea mifupa kwenye chakula chao.
 
DCP wamekunywa sana, nawachanganyia kwenye maji, chakula chao na dagaa wa kutosha!! Tangu nimeanza kuwafuga hivi ni vitu nimekuwa nikizingatia sana.

Nashukuru sana kwa ushauri wako mkuu, nitaendelea kufanya hivyo nione
 
Mi nakushauri rudi kwenye maduka ya vyakula vya mifugo. Waulize kipimo unachotakiwa kuwawekea, kama hawana ugunjwa wowote basi kipimo hakitoshi. Mtafute Amani Ng'oma hapa jf akusaidie
 
Back
Top Bottom