Ligogoma
JF-Expert Member
- Aug 27, 2010
- 3,503
- 6,415
Habari wana JF,
Nafuga kuku wa mayai na wana miezi miwili sasa, tatizo limekuja kwamba wanaanza kupoteza mawasiliano baina ya viungo vyao!! Shingo inapinda na miguu inalegea yaani kiujumla wanakuwa hawawezi kufanya chochote (wanalegea) wanakuwa kama walemavu na kwa sababu wanashindwa kula huishia kufa.
Niliwapeleka kwenye maabara ya mkoa, wakasema kuku wapo vizuri sana na hawana ugojwa but inawezekana hawana vitamin lakini kiukweli nawapa vitamin ya kutosha kabisa, na kwa kufuata maelekezo na vipimo sahihi. Hata nilipowaonyesha wataalam ninavyowapimia wakabaki wanashangaa na kujiuliza tu ni nini??
Nimebaki nabuni tu labda calcium lakini nayo nimekuwa nikiwapa dawa na kuhakikisha chakula chao kina dagaa wa kutosha kabisa!! Labda hewa lakini banda lote kwa juu kwote nimeweka nyavu tu hivyo hewa ni ya kutosha kabisa.
Kwa uzoefu wenu jamani, hili linaweza kuwa ni tatizo gani??