Kuku wanaouzwa kwenye Five star Hotels duniani kote sisi tunadai zina Sumu

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
42,525
Reaction score
74,605
Sisi makabwela tutachelewa sana kutoboa maishani. Tuna jeuri zisizo na msingi wowote. Ni watu wa kupandikiza Hofu kwenye maisha. Hofu zisizo halisi

Kumezuka vijitabia vya sisi makabwela ambao hata mlo miwili tu kwa siku tunaipata kwa taabu tunasema eti Kuku wa Kisasa wana sumu. Kuku hao hao ndio wanaoandaliwa Kwenye Hotel za Kifahari za Matajiri wakubwa. Wanakula Mawaziri wako, Mabalozi, Ma Rais akiwemo na Rais wa Nchi yako.

Wewe kabwela umeshiba viazi unaanza kuzinanga eti hizi Kuku zina Sumu. Najua wasi wasi wako Kabwela unaogopa eti Nguvu za kiume zitapungua maana huna unachokipambania zaidi ya Mauno na kuzaa tu.

Makabwela tubadilike. Huyo Kuku wa Kienyeji abaki kufugwa kama Hobby tu na sio kibiashara. Hatutatoboa.
 
kwenye hili naungana na makabwela wenzangu, hao kuku sio watamu kabisa na hawafai kwa chochote. Kwani kuuzwa kwenye mahoteli ya kifahari ndio maana yake ni salama au halali?
makabwela oyeee,
Au nasema uongo nduguzangu?
 
Pia huku mjini wahindi wanazila sana hizi kuku za kisasa.
Nataka nijue zimewapa madhara gani ya kiafya.?
 
Watanzania wana kasumba ya kuamini kitu fulani hakifai hata ufanye nini hicho kitu hawatakikubali kamwe...mfano mmojawapo wa kitu walichokikataa ni supermarket
 
kwenye hili naungana na makabwela wenzangu, hao kuku sio watamu kabisa na hawafai kwa chochote. Kwani kuuzwa kwenye mahoteli ya kifahari ndio maana yake ni salama au halali?
makabwela oyeee,
Au nasema uongo nduguzangu?
Ni mazoea tuu ndugu, ukizoea wa kisasa utaona wa kienyeji ana radha mbaya.
 
Hawa mawaziri waliotuweka foleni kwenda kwa babu wa Loliondo kunywa Kikombe cha Babu,,, halafu huko 5 Star si ndo viongozi unaowaita akina Dr. Babu Tale naye anaendaga ???
Afya ya mtu ni jambo binafsi na Ushauri huwa si sheria,,, kwani hao matajiri ni wangapi wanakunywa pombe tena kali na kuvuta sigara, kwahiyo we hufahamu kama zina sumu?
Halafu kuna uhusiano gani kati ya Utajiri, Uongozi wa mtu mwingine na Afya yako wewe?
Halafu wale kuku unaowaona pale hawajatoka vichochoroni,, kama ni 5 Star inayojielewa supplier lazima awe anayeeleweka na nyama inapimwa kuangalia kiwango cha sumu kilichopo, siyo kama huku mtaani tunavyouziana maziwa ya NG`OMBE ALIYE KWENYE DOZI..
 
Watanzania wana kasumba ya kuamini kitu fulani hakifai hata ufanye nini hicho kitu hawatakikubali kamwe...mfano mmojawapo wa kitu walichokikataa ni supermarket
Lakini Condomu na P2 sasa
 
Sisi makabwela tutachelewa sana kutoboa maishani. Tuna jeuri zisizo na msingi wowote. Ni watu wa kupandikiza Hofu kwenye maisha. Hofu zisizo halisi

Kumezuka vijitabia vya sisi makabwela ambao hata mlo miwili tu kwa siku tunaipata kwa taabu tunasema eti Kuku wa Kisasa wana sumu. Kuku hao hao ndio wanaoandaliwa Kwenye Hotel za Kifahari za Matajiri wakubwa. Wanakula Mawaziri wako, Mabalozi, Ma Rais akiwemo na Rais wa Nchi yako.

Wewe kabwela umeshiba viazi unaanza kuzinanga eti hizi Kuku zina Sumu. Najua wasi wasi wako Kabwela unaogopa eti Nguvu za kiume zitapungua maana huna unachokipambania zaidi ya Mauno na kuzaa tu.

Makabwela tubadilike. Huyo Kuku wa Kienyeji abaki kufugwa kama Hobby tu na sio kibiashara. Hatutatoboa.
Kitu kuuzwa duniani au nchi nyingi haimanishi hakina madhara , Hata coca cola ipo Takriban kila nchi ila fuatilia madhara ya kunywa coca cola mda mrefu kiafya .
 
Back
Top Bottom