Kuku wangu wana ugonjwa unawatengenezea vidonda puani na masikioni

Philemon38

Member
Joined
May 30, 2018
Posts
74
Reaction score
31
Mimi ni mfugaji wa kuku hapo sina uzoefu sana ila katika zoezi hilo nimekutana na changamoto ya ugonjwa ambao nimeshndwa kuutambua, naombeni ufumbuzi wa hili tatizo wakuu.

IMG_20221012_091903.jpg
IMG_20221012_091658.jpg
IMG_20221012_091851.jpg
 
Ni mafua ya kuku
Tena ni mafua makali pata dawa ya Tylodox, Limoxlin au enrovet

Mgonjwa mgumu kutibaka kama una vifaranga vyote vinaweza kufu.
Macho ya kuku yanaziba anakuwa kipofu
 
Nashukuru sana mkuu ntalifanyia kazi
 
Hiyo kwa uzoefu wangu ni ndui sio mafua. Mafua makali huwa yanaathiri macho tu(yanavimba na/ kuziba kabisa). Ila ndui huathiri maeneo ya wazi ya ndege upande wa kichwani.
 
Tupe tiba rafiki kama unaijua
 
Ndui ya kuku hushusha Sana kinga ya kuku

Nini Cha kufanya

Nunua otc 20% na vitamin Kisha wape kuku wako ili kuboost kinga

Kisha.

Tafuta mafuta ya ng'ombe wapake maeneo yaliyoathirika asubh na jion

Utaona Yale maeneo yaliyoathirika maghamba yanatoka yatoe taratibu

Au

Kama utakosa mafuta ya ng'ombe tumia ya kondoo au maziwa ya fresh ya ng'ombe yasiyo na maji tumia lile tui zito kupaka kwenye vidonda

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
napita kwenye changamoto hii pia,hayo ni mafua makali na nimeokoto vifaranga wafu vyakutosha tu,dawa niliyoanza nayo ni otc 20% na Esb3 walichangamka lakini vifo havikuacha ingawa vilipungua idadi nikabadili dawa to tylodox leo wana siku ya pili na sijaokota vifo
pole mkuu
 
Nadhani ulichoeleza ni sawa ila ningemshauri kununua OTC 50% badala ya 20%.
 
Ni mafua ya kuku
Tena ni mafua makali pata dawa ya Tylodox, Limoxlin au enrovet

Mgonjwa mgumu kutibaka kama una vifaranga vyote vinaweza kufu.
Macho ya kuku yanaziba anakuwa kipofu
We ni daktari?
 
Mkuu hiyo ni ndui ya kuku, (chicken pox) kwa sasa uwezekano wa kupona ni mdogo sabab ni ugonjwa wa virus. Ulichotakiwa kufanya (kabla ugonjwa haujaingia) ni kuchanja chanjo ya ndui ambayo hua inachanjwa vifaranga wakishafikisha umri wa wiki sita.
 
napita kwenye changamoto hii pia,hayo ni mafua makali na nimeokoto vifaranga wafu vyakutosha tu,dawa niliyoanza nayo ni otc 20% na Esb3 walichangamka lakini vifo havikuacha ingawa vilipungua idadi nikabadili dawa to tylodox leo wana siku ya pili na sijaokota vifo
pole mkuu
Baba kama Mafua , chukua magadi , twanga tangawizi mbichi, na pilipili yoyote ,then weka kwenye maji wape wanywe halafu wakimaliza wape glucose utakuja kunishukuru . Hii dawa inatibu kuharisha namafua mara moja al
 
Nashukuru sana mkuu ntalifanyia kazi
Sio mafua hayo,hio ni ndui na haina tiba inahitaji chanjo.Unachoweza fanya hapo pata spirit gandua hivyo vidonda kisha safisha kwa spirit.Mara nyingi kama utakua makini kwenye kuwasafisha mara kwa mara watapona.Zingatia kuwapa dawa za vitamini zitawapunguzia stress na kuongeza hamu ya kula.
NOTE,
Chanjo hutolewa kwa kuku wazima,kwa hao,watibu kwanza wakishapona ndipo uwachanje.Kimsingi huu ni ugonjwa wa virusi hauna tiba,tunachofanya hapa ni kuhangaika na kutibu zao la ugonjwa mfano hivyo vidonda na kuku anaweza kupona kwa ndui si issue sana.Kwa kideri ndio tatizo ila ndui mara nyingi ukikomaa nao wanapona
 
Ninaposoma comment za watu humu ninachogundua watu waliowengi ni watupu sana kwenye ufugaji.Tujitahidi sana walau kusoma vijarida vya ufugaji ili tupunguze hasara.
Kwakweli comment nyingi zinanifikirisha sana.
 
Vema ungechangia nawewe kumsaodia ndugu mfugaji halafu mwisho ungekosoa

Sawa tumekosea haya tupe maoni yako

Back
Top Bottom