Kuku wangu wana ugonjwa unawatengenezea vidonda puani na masikioni

Kuku wangu wana ugonjwa unawatengenezea vidonda puani na masikioni

Kama walivyoeleza wachangiaji wengine.
Huo ni ugonjwa unasababishwa na virusi( (an avipoxvirus in the Poxviridae family).
Na huenezwa haswa na mbu waumao(Culex ), kama eneo linalokuzunguka kuna mbu wengi, tambua ya kwamba upo kwenye eneo ambalo ni rahisi sana ugonjwa kuenea kwa haraka.

Ugonjwa wa Ndui una chanjo yake(Fowl pox vaccine).
Chanjo hii hupatiwa kifaranga kuanzia wiki ya 5-8 , ni vizuri ukawahi mapema kuwachanja kabla ya ugonjwa haujaingia bandani mwako.,
Hii chanjo ni ya kuchoma hivyo basi ni vizuri kupata ushauri kutoka kwa daktari wa Mifugo aliyekaribu Yako .

Ugonjwa huu hauna Tiba pale utakapowapata vifaranga, lakini inashauriwa kuwapa antibiotics kwaajili ya kumsaidia kifaranga asipatwe na magonjwa mengine nyemelezi( kumbuka virusi hivi huzoofisha Kinga ya mwili, hivyo basi ni rahis sana kifaranga kuanza kushambuliwa na magonjwa mengine)

Antibiotics hizo ni kama OTC 20% , OTC 50% na Amoxycol.
Mimi napenda sana kushauri mfugaji atumie Amoxycol kwani husaidia kukausha vidonda(local inflammations), husaidia kuzuia magonjwa nyemelezi hasa Yale yatokanayo na virusi kama Ndui, mdondo(Newcastle) na Gumboro.

Usichubue vidonda pale vitakapotokeza, ni Bora kutumia dawa na kupata ushauri.
Kumbuka kuwapatia na multivitamins kusaidia kupunguza stress zitokanazo na ugonjwa.

Kinga ni Bora kuliko Tiba.
MIFUGO NI MALI 🐥🐣🦃🦢🐖🐄🐕‍🦺
 
Ndui ya kuku hushusha Sana kinga ya kuku

Nini Cha kufanya

Nunua otc 20% na vitamin Kisha wape kuku wako ili kuboost kinga

Kisha.

Tafuta mafuta ya ng'ombe wapake maeneo yaliyoathirika asubh na jion

Utaona Yale maeneo yaliyoathirika maghamba yanatoka yatoe taratibu

Au

Kama utakosa mafuta ya ng'ombe tumia ya kondoo au maziwa ya fresh ya ng'ombe yasiyo na maji tumia lile tui zito kupaka kwenye vidonda

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Barikiwa sana
 
Back
Top Bottom