Kuku wangu wana ugonjwa unawatengenezea vidonda puani na masikioni

Kama walivyoeleza wachangiaji wengine.
Huo ni ugonjwa unasababishwa na virusi( (an avipoxvirus in the Poxviridae family).
Na huenezwa haswa na mbu waumao(Culex ), kama eneo linalokuzunguka kuna mbu wengi, tambua ya kwamba upo kwenye eneo ambalo ni rahisi sana ugonjwa kuenea kwa haraka.

Ugonjwa wa Ndui una chanjo yake(Fowl pox vaccine).
Chanjo hii hupatiwa kifaranga kuanzia wiki ya 5-8 , ni vizuri ukawahi mapema kuwachanja kabla ya ugonjwa haujaingia bandani mwako.,
Hii chanjo ni ya kuchoma hivyo basi ni vizuri kupata ushauri kutoka kwa daktari wa Mifugo aliyekaribu Yako .

Ugonjwa huu hauna Tiba pale utakapowapata vifaranga, lakini inashauriwa kuwapa antibiotics kwaajili ya kumsaidia kifaranga asipatwe na magonjwa mengine nyemelezi( kumbuka virusi hivi huzoofisha Kinga ya mwili, hivyo basi ni rahis sana kifaranga kuanza kushambuliwa na magonjwa mengine)

Antibiotics hizo ni kama OTC 20% , OTC 50% na Amoxycol.
Mimi napenda sana kushauri mfugaji atumie Amoxycol kwani husaidia kukausha vidonda(local inflammations), husaidia kuzuia magonjwa nyemelezi hasa Yale yatokanayo na virusi kama Ndui, mdondo(Newcastle) na Gumboro.

Usichubue vidonda pale vitakapotokeza, ni Bora kutumia dawa na kupata ushauri.
Kumbuka kuwapatia na multivitamins kusaidia kupunguza stress zitokanazo na ugonjwa.

Kinga ni Bora kuliko Tiba.
MIFUGO NI MALI πŸ₯πŸ£πŸ¦ƒπŸ¦’πŸ–πŸ„πŸ•β€πŸ¦Ί
 
Barikiwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…