Kuku wangu wanataga na hakuna jogoo. Je, kuna uwezekano wa mayai kuanguliwa?

Kuku wangu wanataga na hakuna jogoo. Je, kuna uwezekano wa mayai kuanguliwa?

Trainee

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
2,660
Reaction score
3,501
Habari zenu,

Nina kuku wa kienyeji hapa kwangu ambao nimewazuia wasizagae mtaani, sasa wiki hii kuku wote wakubwa wameanza kutaga na hapa sina jogoo hata mmoja.

Je, niendelee kula haya mayai au niwaachie kuna uwezekano wa kuja kuanguliwa?
 
Kuku wanataga mayai hakuna hata jogoo inakuwaje, sio bure kuna likuku huwa tena nahisi mida ya usiku usiku😂
 
Kuku wanataga mayai hakuna hata jogoo inakuwaje, sio bure kuna likuku huwa tena nahisi mida ya usiku usiku😂

Yai linaweza kutagwa bila jogoo...jogoo kitu pekee anafanya ni kuhamisha chromosomes kwenda kwenye yai teke lililo mwilini mwa kuku jike ili kuunda kiumbe kitachokua ndani ya yai pindi litapotagwa...

Hata wanawake huwa wanadondosha yai/mayai kila mwezi na hutolewa na damu ya hedhi kama hayajarutubishwa na mbegu za kiume...

Yai ni seli inayojitegemea...
 
Kuku wanataga mayai hakuna hata jogoo inakuwaje, sio bure kuna likuku huwa tena nahisi mida ya usiku usiku😂
Kuku wanao uwezo wa kutaga mayai bila kupandwa na jogoo.
Ila hayo mayai yanakuwa hayana mbegu ya jogoo so huwezi kuyatotolesha yanafaa kwaajili ya kula tu.
 
Kiwa makini na huyo dogo anaewahudumia kuku isije kuwa unaka watot wake😁😁
 
bila jogoo hawawezi kutotoa we kula tu mayai au wapeleke kwa jirani kama kuna jogoo awapande
 
Kwan anaeatamia si ni mtetea? Sasa jogoo hapo wa nini?
 
IMG_0789.jpg

Njoo kwangu uchukue jogoo mambo yawe vizuri
 
Back
Top Bottom