Kuku wangu wanataga na hakuna jogoo. Je, kuna uwezekano wa mayai kuanguliwa?

Kuku wangu wanataga na hakuna jogoo. Je, kuna uwezekano wa mayai kuanguliwa?

Yai linaweza kutagwa bila jogoo...jogoo kitu pekee anafanya ni kuhamisha chromosomes kwenda kwenye yai teke lililo mwilini mwa kuku jike ili kuunda kiumbe kitachokua ndani ya yai pindi litapotagwa...

Hata wanawake huwa wanadondosha yai/mayai kila mwezi na hutolewa na damu ya hedhi kama hayajarutuboshwa na mbegu za kiume...

Yai ni seli inayojitegemea...
Nimeongeza maarifa. Thanks
 
Alooo kumbee, sikujuaga hili jambo.

Vipi kuku wa kisasa hawa bloila sijui nao wanaweza kupandwa na yai lake likatotoleshwa, au wao ni kutaga yai tu liliwe??
 
Habari zenu

Nina kuku wa kienyeji hapa kwangu ambao nimewazuia wasizagae mtaani, sasa wiki hii kuku wote wakubwa wameanza kutaga na hapa sina jogoo hata mmoja

Je niendelee kula haya mayai au niwaachie kuna uwezekano wa kuja kuanguliwa?


Kwanini usiwatafutie jogoo (mme) wao??!!, au unataka wawe mashoga??!!
 
Kuku jike huwa anatengeneza mayai na kuyataga bila shida ila hayawezi kutotoa vifaranga sababu hayana mbegu ya jogoo.

Ili yai liweze kutengeneza kifaranga ni lazima jogoo ampande arutubishe yai na kuweza kutengeneza kifaranga ndani ya yai. Hapo akitaga ana atamia ili kulipa joto yai liweze kuumba kifaranga.
 
Back
Top Bottom