Alvin Slain
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 6,375
- 3,663
- Thread starter
-
- #21
Inaitwa KEPROCERYL (Hydrosoluble mix of antibiotics and vitamins). Angalia expire date, kuna mtindo wa kuuza dawa zilizoisha muda wake wa matumizi.
swali uliwapa chanjo?
Apolinary Pole sana mkuu,
nasikitika sikuiona hii post yako mapema, ila napenda kukupa ushauri
chukua kuku mmoja ama wawili wahi ahsubuhi na mapema uwapeleke veterinary (Wizara ya mifugo) maeneo ya Tazara, ukifika pale getini watakuelekeza cha kufanya. ila Nikufahamishe ni kwamba kuku hao watapelekwa maabara kupasuliwa na kuchunguzwa tatizo lao ili watoe ushauri wa dawa utakayotumia. Ada yao nahisi si chini ya shs 3000/- inaweza kuwa imepanda.
Ushauri huu unahusu kuku wa kisasa na kienyeji, tena ifikapo wiki ya tatu au ya nne peleka kuku pale wakawaangalie na kushauri chanjo inayofuata ama lolote lile. Kama unatumia chakula spesheli peleka sample nayo ili wakague nini kimekosekana na nini kimezidi ili wakushauri aina ya chakula unachopaswa kutumia kwa aina ya kuku ulionao.
Hatari ya kwenda duka la madawa bila prescription ya wataalam ni kucheza bahati nasibu.
hawa kuku mdomoni wana kama majimaji au kamasi!!! halaf wanakoroma!!!
Kideri hicho dogo; hukuwachanja ndo maana wameugua. Nakushauri uwauze wote upate hela ukaanze upya. Magonjwa mengine yanavumilika lakini kideri ni noma.
Yaani wewe acha
Kila siku ni kuku watano wanakufa,
Lakini jana nimewapeleka Sokoni nikawapigs bei wote sasa nianze upya
Unawafugia bandani au wanatembea nje?
Ukileta wengine hakikisha kwanza unafanya usafi wa kutosha kwenye mabanda kabla ya kuingiza kuku wapya. Bei ya kuku huko ikoje?

Bei ya kuku mtetea kwa wastani ni 8,000
Lakini Jogoo ni kuanzia 10,000 mpaka 15,000
Kwa maeneo mengi Arusha.
Je kuna dawa za kupuliza kwenye banda ili niweze kuweka kuku wapya!!!
mbona bei chini sana wakati naambiwa maisha ya Arusha yako juu? Hapa Mwanza mitetea tshs. 10,000 hadi 12,000/ majogoo Tshs 15,000 - 20,000 kutegemeana na ukubwa wa kuku

Inategemea na soko sio kote bei ziko hivyo!
Mimi huwa nanunua soko la mkuyuni kuku wa kitoweo Tetea napata kwa 7000-8000 na kuna kipindi nilikuwa nachukua hadi kwa 6000!
Ila Kirumba na mjini hizo ndo bei zake!
Je kuna dawa za kupuliza kwenye banda ili niweze kuweka kuku wapya!!!
osha vyombo kilasiku, usiruhusu mtu kuingia bandani, weka maji ya dawa (deto,mafuta ya taa) kwenye karai ili mtu akiingia akanyage kwanza humo. pia pawe na viatu maarumu hata kwako unapotoka nje ya kwako ukitaka kuingia bandani uvae