Kukua kwa miji na kumezwa vijiji vya wakulima (urbanisation at the expense of peasants livelihood) Tanzania

akitendewa hivyo anayekuhusu, baba, mama, kaka, dada utafurahi? au unasema kwa vile umebahatika na hivho ulichonacho (kama kipo anyway)
Kwahyo tuendelee kuwa na mashamba mjini? Ni sawa na serekali ingeendelea kuwa na nyumba za miti kariakoo. Kunawakati kama wewe n mtu muelewa hata kama unashamba mjini, ni Jambo la muda tu lazima kunawakati utalazimishwa kuuza kama hukuchukua maamuzi mapema. Maeneo ya kulima yapo mengi tu kwa hiyo mwenye shamba hanyang'anywi Bali atauza
 
Moja ya ujinga wa hali ya juu ni hili lla kuchukua ardhi ya wakulima wadogo kiholela na kwa kasi na kupima viwanja vya .makazi. Kwanza wanachochea na kuongeza tatizo la ajira, hao wakulima wanaoporwa mashamba yao wanakuwa hawana njia ya kipato hivyo kuongeza matatizo ya kijamii kama wizi, umalaya na uhalifu mwingine pamoja na kufanya familia nyingi zitegemee uchuuzi kama njia ya kuishi; halafu hao hao viongozi wanashangaa machinga kuongezeka mijini na kuwafukuza wanasahau kuwa ni wale walionyang" anywa masha.mba yakapimwa viwanja. Wizara yenyewe inajinasibu kuwa wanaingiza mabilioni kama kodi ya ardhi kila mwaka kwa kuongeza viwanja vilivyopimwa lakini wanasahau kuwa ardhi hiyo hiyo ilikuwa inazalisha mapato zaidi ya hiyo kodi ya ardhi ambayo ni kipato cha moja kwa moja kwa familia zinazolima katika ardhi hiyo, mkulima analima na kuvuna mara mbila kwa,mwaka au hata,mara tatu halmashauri zinapata kodi kwa njia ya ushuru wa mazao yaliyokuwa yakliimwa katika viwqnja hivyo wakati havijapimwq.

Kwa kupima viwanja holela tunatengeneza taifa la fanilia ambazo ni jobless, au zinategemea umachinga, bodaboda, umalaya misheni town ili kuishi. Umaskini ule abject poverty hauwezi kuisha.

Kiuchumi huwa tunashugulika zaidi na employment kati ya natatizo mbalimbali ya nchi kwa sababu inaleta stability katika nchi na kuondoa political and social turmoils ndio maana nchi zilizoendelea ziko makini sana na vitu vinavyotemper au kusababusha ajira zipotee. Pia watu wakistaafu kazi kutokana na pensheni kiduchu hutegemea kujikimu kwa kulima sasa kwa kasi hii ya upimaji hawatakuwa na mashamba ya kulima hivyo kushindwa kumudu maisha baada ya kustaafu kumbuka hata bima ya afya wanabanwa sana kwa kuondolewa matibabu muhimu hivyo kutegemea kipato ili wasurvive kiafya; sasa kwa mwendo huu wa kunyang'anywa ardhi watasbindwa kuendesha maisha yao hivyo kufa mapema.

Wako watu watakuja na argument za ujenzi holela lakini waelewe nchi hii imeshindwa kulinda ardbi ya kilimo cha wakulima wadogo na inafanywa makusudi. Ardhi yote ya wakulima wakubwa inalindwa kisheria na imepimwa na hao hao wizara ya ardhi na hata kuwe na uhitaji namba gani wa viwanja haIguswi.

Japan ni nchi ndogo mara nane ya Tanzania lakini ni vigumu sana kubadili ardhi yake ya kilimo kuwa makazi ingawa wako wengi kama mara mbili ya watanzania..

Uzalendo na kufikiri criticalky ni tatizo kubwa kwa wenye nafasi mbalimbali za maamuzi.
 
asante kwa observation nzuri sana
 
Sasa Mji ukihitaji makazi inakuaje? Kama ni kulima watalima pembeni ya Mji ,ukikua na kuwakuta tena wanapisha hivyo hivyo..

Sasa unataka iwaje?
 
Hii ndio point
 
Hapana ,ukichukua ardhi yao ni ama walipwe fidia au watakonunua wao wenye mashamba wawe na 50% ya thamani ya plots Ili sasa kuwawezesha kwenda Nje ya Mji.kununua maeneo Mengine au kubadili shughuli za uchumi.
 
Sitaki kuamini kuwa kwenye hizo master plans za miji yetu hakuna mgawanyiko wa kuonyesha maeneo ya mashambani na ufugaji
 
Sasa Mji ukihitaji makazi inakuaje? Kama ni kulima watalima pembeni ya Mji ,ukikua na kuwakuta tena wanapisha hivyo hivyo..

Sasa unataka iwaje?
Miji inakua kwa kujenga viwanda, siyo kuwanyanganya watu ardhi yao kukata viwanja kuwauzia wanaokimbia vijijini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…