Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 224
- 236
Anaandika Mo Mlimwengu.
Kwanza nitoe pongezi kwa Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuanzia kwa Mwenyekiti , watendaji wa chama pamoja na wanachama wote. Uimara wenu ndio unasababisha hadi leo hii CCM kinabaki kuwa chama tawala tangu tupate uhuru. Tumeishashuhudia vyama vingi kwa Afrika ambavyo vilipigania uhuru lakini tayari havipo madarakani.
Ninaandika waraka huu kwa kutoa maoni yangu juu ya demokarasia kwenye chama chetu. Ninatambua kwamba Chama chetu kina misingi ya ujamaa ambayo inazingatia usawa na utu kwa kila mtu. Tunapoenda kwenye uchaguzi wa 2025 kuna vitu inabidi viboreshwe isiwe kama uchaguzi wa 2020. Kitu cha kwanza ni namna ambavyo kwa nafasi ya ubunge na udiwani kutumia wajumbe tu kwenye kura za maoni. Haya ni madhara ya kuwatumia wajumbe badala ya kutumia wanachama wote;
Kuchochea rushwa, kitendo cha kutumia wajumbe tu kinasababisha rushwa ikithiri kuliko kawaida. Hapa wajumbe wanachoangalia ni kwamba mwenye anatoa kiasi kikubwa kwa rushwa ndio anachagulika. Na hii tuliona kwenye uchaguzi wa 2020. Hii inapelekea kutoa ushindani wa kisiasa bali inakuwa ushindani wa misuli ya fedha. Kwa mantiki hii hata ambao wanatetea maeneo yao ya kiungozi na ambao wanataka kugombea inawafanya wamjali zaidi mjumbe anayewapigia kura na kuwaacha idadi ya wanachama wengi wakiwa yatima.
Kupunguza idadi ya vijana kwenye uongozi, asilimia kubwa ya vijana ambao wana uwezo mzuri wa masuala ya uongozi wa kisiasa kukosa fursa hiyo. Vijana wengi bado hawajawa na ukwasi wa kutosha wa kuwahonga wajumbe. Hii inapelekea tupate viongozi ambao kwa kuwa wana hela za kutosha. Wanapata nafasi ambazo zitawasaidia kuwanufaisha wao binafsi kuliko kuangalia watu ambao wanawaongoza. Kwa mantiki hii tutapata wawakilishi ambao ni wezi, mafisadi na ambao watakuwa wafujaji wa mali za umma. Hapa simuoni kijana kwenye vyombo vya maamuzi. Hapa vijana wataishia kuwa wapiga debe wa wagombea na kutetea watu ambao ni kikwazo kwa maendeleo ya taifa letu.
Kupunguza wananchi kukipigania chama, hii tutapunguza idadi ya wanachama kwa kuwa wanaona wao siyo sehemu ya maamuzi kwenye kuchagua viongozi wao. Mwanachama atajiuliza kuna haja gani ya kuwa na kadi ya chama wakati kwenye maamuzi hatushirikishwi? Wataona ni bora kuwa na kadi ya kupigia kura kuliko kuwa mwanachama. Na baadhi ya wanasiasa wababaishaji wanaonyesha kuwatenga wanachama wengine na kuzingatia zaidi hao wajumbe ambao wanaamini ndio wapiga kura wao. Hii inapunguza morali na baadae inaweza kuleta madhara baadhi ya watu wakaacha kuhudhuria mikutano ya viongozi.
Kupata viongozi mizigo, wajumbe ni idadi ya watu watu wachache kwenye jamii husika. Sisi siyo kama mataifa ya wenzetu yaliyoendelea kama China au Singapore. Kule wanatumia wajumbe wachache ambao wana maarifa ya kutosha. Ashakum si matusi ila kwenye maeneo yetu mengi tuna viongozi wa chama(wajumbe) ambao hawana ueledi na hao hao ndio wana maamuzi ya kutuchagulia viongozi wakutuwakilisha. Asilimia kubwa ya wajumbe ni madalali wa wagombea. Hii inapelekea tupate viongozi ambao hawana ueledi.
Kupunguza wanachama wa CCM, tutakuwa na wanachama ambao wana kadi ambazo siyo hai hawataweza kuzilipia kwa sababu hazina kazi kwao. Kitendo cha wanachama wote kupiga kura wataanza kulipia ada ili waweze kuhusika kwenye kuchagua viongozi wao.
Wagombea kuelezea ajenda wanazokusudia kufanya kwenye nafasi zao. Hii itawasaidia kuzunguka maeneo mengi na kunadi sera zao ambazo zitapelekea wachagulike na wananchi. Na huo uzoefu utaweza kusaidia kwa ambao wamepatikana kuweza kushindana na vyama vingine vya upinzani baada ya kura za maoni