Kukuza uchumi wa nchi yetu katika kilimo

Joined
May 8, 2014
Posts
73
Reaction score
10
Kilimo ni mojawapo ya njia ya kukuza na kuinua uchumi wa nchi yetu, lakini bado wakulima wanapata shida kubwa sana katika mambo mbalimbali ikiwemo.

Kukosa wataalam na washauri wa mbegu bora, changamoto za kupata mbolea na kikubwa zaidi kukosa soko la uhakika ya kuuza mazao.

Naamini kuwa serikali ikituboreshea masoko ya mazao uchumi na kipato cha nchi yetu itaongezeka.
 
Ulikua unajaribu kutoa wazo, ushauri, maoni, ombi au nini?

Anyway, kuna vitu vingi vya kuamini, lakini sio hivyo hapo kwenye Blue, sio kwa serikali hii ya sasa!!
 
jaman hapa tz twatakiwa kufanya kilimo kwa akili kwan tukijikita tu kulima bila kuangalia nn tunazalisha na kwa gharama zipi tutaumia tu,kwani yapo mazao yanayozalishwa yaan hayana tija kabisa
 
Kwa kuwa hii ni Forum, ngoja tuandike,

Wahenga walisema "Umoja ni Nguvu, Utengano ni Udhaifu". Ifike Wakulima waungane. Hapa nina maanisha Umoja halisi sio umoja wa Vyama vya Ushirika tunavyoviona leo kama vya KCU, NCU, n.k.

Ninaamini Wakulima wodogo wadogo, yaani wenye mitaji midogo wakiungana wanaweza kutetea haki zao, kupambana na utapeli na dharau kubwa inayoendeshwa na Serikali, Madalali wanajiita Wafanyabiashara na Taasisi nyingine nyingi. Hili linawezekana.

Ninaamini Wakulima wa Kati wanaweza kuunda Umoja wao vile vile na kupata manufaa kama niliyoyataja hapo juu.

Sambamba na hao, Wakulima wakubwa, kama wapo, wanaweza kufanya hivyo hivyo.

Kwa Wakulima Wadogo na wa Kati Umoja wao unaweza kuwa katika ngazi ya eneo walilomo, yaani Wilaya hata Mkoa. Hili linawezekana kabisa.

Kama sehemu ya Forum hii, huwa ninatamani sana wenye Ujuzi wa Sheria watueleweshe Sisi Wana-Umma ni Sheria zipi zinatumika kumzuia Mkulima mdogo asiuze Mazao yake nje ya Wilaya/Mkoa wake. Mpango wa Biashara Huria una Mipaka gani, kwa nini Wakulima wawekewe mipaka na vikwazo kibao? :A S confused:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…