SI KWELI Kukwangua vocha kwa vidole ni hatari kunasababisha kansa kwa sababu zina kemikali ya Silver Nitro Oxide

SI KWELI Kukwangua vocha kwa vidole ni hatari kunasababisha kansa kwa sababu zina kemikali ya Silver Nitro Oxide

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
ATTENTION!
Medical research authority of the US have found new cancer in human being caused by silver nitro oxide.

Whenever you buy recharge cards dont scratch with nails as it contains
silver nitro oxide coating and can cause skin cancer.

Share this msg with your loved ones.
---
Naye Bata batani mwaka 2012 aliuliza:
Jamani hapo jana nilitumiwa sms hii kwenye simu yangu na inasema hivi:

"Tahadhari marekani wamegundua ugonjwa mpya wa kansa unapatikana kwa mwanadamu unaosabishwaa na SILVER NITRO OXIDE ambayo inatoka kwenye unga wa vocha kwa hiyo hakikisha unaponunua vocha unapokwangua vocha na kucha unga ule wa vocha usikuangukie kwani unasabisha kansa ya ngozi tuma sms hii kwa watu wengine"

Je kuna ukweli wowote juu la hiliii maana sms hii imesambaaa kwa watu wengi
1705294365087.png
 
Tunachokijua
Tangu mwaka 2011 kulikuwa na ujumbe uliokuwa unasambaa mitandaoni hasa FaceBook na WhatsApp ukitahadharisha tabia ya watu kukwangua vocha kwa kutumia kucha zao kwa madai zina kemikali inayoitwa Silver Nitro Oxide inayoweza wasababishia kupata kansa ya ngozi. Ujumbe huo unaeleza kuwa Madaktari Marekani wamebaini kuwa vocha ina kemikali ya Silver Nitro Oxide inayosababisha kansa ya ngozi.

JamiiCheck imefatilia vyanzo mbalimbali na kubaini kuwa kwamba ujumbe huo ulianza kusambaa mitandaoni mwishoni mwa mwaka 2011 na kusambaa zaidi kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2012 na kuendelea baada ya kuanza kuchapishwa na kutafitiwa na kurasa mbalimbali.

Aidha, JamiiCheck pia imebaini kuwa baada ya Ujumbe huu kusambaa mashirika mbalimbali ya uhakiki wa habari yakiwamo AFP, The New India Express, Consumerizim, 211 Check, ambao wamefanya uchunguzi na kubaini kuwa madai hayo hayana ukweli. Katika uchunguzi wao wote wamebaini kuwa hakuna kemikali ya Silver Nitro Oxide katika kadi za vocha kama ujumbe huo unavyodai.

Mathalani, katika uchunguzi wa AFP wanaeleza kuwa
Madai kuhusu kuwapo kwa aina mpya ya kansa ni ya uwongo; wataalam waliwaambia AFP Fact Check kupitia barua pepe Juni 13, 2020 kwamba "Hakuna kemilaki inayoitwa'silver nitro oxide'" msemaji wa Shirika la Ulinzi wa Mazingira la Marekani (EPA).
AFP Fact Check ilifanya utafutaji wa rekodi katika database ya Wakala wa Kimataifa wa Utafiti juu ya Kansa (IARC), shirika la serikali linaloendeshwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linaloratibu utafiti kuhusu visababishi vya kansa lakini katika orodha yake hiyo hakuna kemikali ya Silver Nitro Oxide inayotajwa.
Nao, 211 Check hawatofautiani na AFP ambao katika uchunguzi wao pia wamebaini kuwa hakuna kemikali inayoitwa Silver Nitro Oxide ambapo wao wamefanya utafiti wao kwa kuwahusisha wataalamu wa kutengeneza madawa na kemikali PubChem na ChemSpider ambao pia wanafafanua kuwa hakuna kemikali yoyote inayoitwa Silver Nitro Oxide.

JamiiCheck pia imepitia ukurasa wa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (CDC) ambao wao wanaeleza kuwa Kansa ya ngozi inasababishwa zaidi na miale ya jua na vyanzo vingine lakini haijataja kabisa kuhusu kemikali ya Silver Nito Oxide.

Hivyo kutokana na hoja na tafiti hizo JamiiCheck inakubali kwamba hoja inayodai kukwangua vocha kwa kucha kunaweza kusababisha kansa haina ukweli.
dah! ngoja wataalam wakuje kutujuza hii kitu...
 
hebu labda TBS waje watueleze kwamba coating layer ya vocha imetengenezwa na nn? nijuavyo mm silver nitro oxide ni kemikali mbaya sana hasa ikitumiwa unwisely. anyway labda watueleze na hata ofisi ya mkemia mkuu waje watuambie kama ni kweli ama la.

nimesoma chemistry lakini sijawahi kusikia kitu kama hicho.labda chemistry imebadilika sana miaka hii
 
Mi sijasikia kuhusu huo ugonjwa ila nishasikia kuwa haifai kukwangulia voucher kutumia kucha za vidole maana zile chembe chembe zina madhara..
 
Hiyo text ya siku nyingi sana.. Yaelekea unakaa mbali sana ndo umekufikia jana!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Husomi magazeti!, hiyo habari iliandikwa na gazeti la jumapili moja kati ya August au September 2012

jamani hapo jana nilitumiwa sms hii kwenye simu yangu.......na inasema hivi:

"Tahadhari marekani wamegundua ugonjwa mpya wa kansa unapatikana kwa mwanadamu
unaosabishwaa na SILVER NITRO OXIDE ambayo inatoka kwenye unga wa vocha kwa hiyo
hakikisha unaponunua vocha unapokwangua vocha na kucha unga ule wa vocha usikuangukie
kwani unasabisha kansa ya ngozi tuma sms hii kwa watu wengine"

je kuna ukweli wowote juu la hiliii maana sms hii imesambaaa kwa watu wengi
 
Mi sijasikia kuhusu huo ugonjwa ila nishasikia kuwa haifai kukwangulia voucher kutumia kucha za vidole maana zile chembe chembe zina madhara..
 
Ccm inasababisha kansa ya ubongo na mnaichekea, mnaogopa vocha. Some pipo banaa
 
jamani hapo jana nilitumiwa sms hii kwenye simu yangu.......na inasema hivi: "Tahadhari marekani wamegundua ugonjwa mpya wa kansa unapatikana kwa mwanadamu unaosabishwaa na SILVER NITRO OXIDE ambayo inatoka kwenye unga wa vocha kwa hiyo hakikisha unaponunua vocha unapokwangua vocha na kucha unga ule wa vocha usikuangukie kwani unasabisha kansa ya ngozi tuma sms hii kwa watu wengine" je kuna ukweli wowote juu la hiliii maana sms hii imesambaaa kwa watu wengi
Post #5 amekujibu kwa kutafuta maelezo yaliyopo online,ndo uzuri wa JF. Kwa kuwa makampuni haya ya simu ni mulitinational naamini watadiriki kuweka kemikali zenye madhara lakini la pili ni kuwa Watanzania tunapokea mambo harakaharaks bils hata kutafakari na ndo kila mahali sasa ni U freemason,viungo vya albino N.K.
 
jamani hapo jana nilitumiwa sms hii kwenye simu yangu.......na inasema hivi:

"Tahadhari marekani wamegundua ugonjwa mpya wa kansa unapatikana kwa mwanadamu
unaosabishwaa na SILVER NITRO OXIDE ambayo inatoka kwenye unga wa vocha kwa hiyo
hakikisha unaponunua vocha unapokwangua vocha na kucha unga ule wa vocha usikuangukie
kwani unasabisha kansa ya ngozi tuma sms hii kwa watu wengine"

je kuna ukweli wowote juu la hiliii maana sms hii imesambaaa kwa watu wengi

Kwa nini bado hawajagundua kwamba wao ndio walioanzisha AIDS walipokuwa wanafanya research for a biological weapon against their enemies. Yes,friends,the US Army invented AIDS.
 
hebu labda TBS waje watueleze kwamba coating layer ya vocha imetengenezwa na nn? nijuavyo mm silver nitro oxide ni kemikali mbaya. anyway labda watueleze na hata ofisi ya mkemia mkuu waje watuambie kama ni kweli ama la.

Waje wapi sasa? kwani TBS na ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali ni members wa JF? Ungekuwa msamaria mema ungeenda kuwauliza afu utuletee majibu hapa ili sisi vichwa maji tupate kuelewa.

Kama vipi Ujanja ni kununua airtime kwa MPesa, Tigo pesa et el.
 
Nijuavyo mm c rahc hawa wenye kampun kukbali. Yaani wathungu wapo kutumaliza. Kikubwa ni kuchkua tahadhari kabla ya hatari.
 
ndio maana nchi nyingi pia hutumia machine maalumu au simu ku load airtime kwenye simu.Bora hiyo sheria ipitishwe TZ kuepusha na hilo janga hata kama ni fununu!
 
Nitro haiwezi exist with an oxide... Thats chemistry.... So hakuna compound kama silver nitro oxide
 
Waje wapi sasa? kwani TBS na ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali ni members wa JF? Ungekuwa msamaria mema ungeenda kuwauliza afu utuletee majibu hapa ili sisi vichwa maji tupate kuelewa.

Kama vipi Ujanja ni kununua airtime kwa MPesa, Tigo pesa et el.
hahahahha! mzima weye Asprin????
nakumisije sasa? ila aliyekuficha this time amekuweza full kukaa chimbo sijui ni mavibration na mfyonzo umezidi huko ama ni deki?
 
Last edited by a moderator:
Nitro haiwezi exist with an oxide... Thats chemistry.... So hakuna compound kama silver nitro oxide

Are u sure mkuu kuhusu hilo? Nitakupa mbili, nitro oxide (NO) a potent vasodilator na nitrous oxide(N2O) hiyo 2 ni subscript nimeshindwa kuiweka sawa kwa sababu natumia mchina, a well known inhalational anaesthetic used in operating theatres
 
hebu labda TBS waje watueleze kwamba coating layer ya vocha imetengenezwa na nn? nijuavyo mm silver nitro oxide ni kemikali mbaya sana hasa ikitumiwa unwisely. anyway labda watueleze na hata ofisi ya mkemia mkuu waje watuambie kama ni kweli ama la.

tbs hii ninayoijua mm au nyingine? kama hii ya bongo andika NIMEUMIA kwa capital letter like what i did
 
Back
Top Bottom