Kula gwala mwanangu

Kula gwala mwanangu

Jemedal_bin_chichi

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
542
Reaction score
585
HAINIPUNGUZII chochote nikikusalimu kwa kukupa gwala asubuhi leo, ila ni nyongeza tu ya uungwana. Kula gwala mtu wangu!

Gwala nikupazo ni mambo matano yaliyotikisa jana kutoka duniani kuja Tanzania na kutoka Tanzania kwenda duniani. Kula gwala za jana ili tufunge hesabu ya jana kisha tuianze leo tukiwa fresh! Tukijaa matumaini kede wa kede.

MOSI: Ni lile shambulio la aibu ambalo Barca wa Catalonia waliwafanyia vibosile wa Madrid. Barcelona walitumbukiza mabao Hamsa ndani ya nyavu za Real Madrid, kisha Madrid wakatupiamo Kamoja kepeeesi! Hamsa kwa Waheda za Mwana Ukome!

Ushauri kwa RC wetu Makonda, aagize Barcelona waripoti kituo chochote cha polisi Dar kabla ya saa 12 jua la Magharibi leo ili haki itendeke. Maana vipigo kama vile ni mali ya jamhuri, hairuhusiwi kwa watu binafsi.

PILI: Hattrick ya Louis Suarez. Inaweza kumfanyia Wema Sepetu masahihisho ya ubongo. Ikamuondolea uzwazwa, muwasho na mawenge ya Kishetani na kumpa utulivu wa Kimalaika.

TATU: Kuna miungurumo mitano ya kutisha ilitokea Uwanja wa Taifa. Ni miungurumo ya Simba. Ikasababisha nchi itetemeke. Ikadhaniwa mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto yamelipuka tena kwa wakati mmoja. Kumbe Simba ilikuwa inawaungurumia Ruvu Shooting, wakati ilitakiwa kuwapapasa tu. Miungurumo Mitano Bila.

Mpaka sasa nanusa harufu ya upendeleo. Sijasikia agizo la RC Makonda kutaka Simba waripoti kituo chochote cha polisi Dar leo kabla ya saa 12 jioni. Simba washitakiwe aisee!

NNE: Hattrick ya Emmanuel Okwi. Inaweza kumsafirisha Amber Rutty kutoka Tanzania ya Karne ya 21 mpaka Jordan ya milenia nyingi zilizopita ili akashuhudie kwa macho sababu ya watu wa Luttu kulaaniwa katika miji ya Sodoma na Gomora. Labda atajifunza.

TANO: Press Conference ya Zitto Kabwe. Nondo kwa nondo bila ufa, ukuta wa Berlin chamtoto. Zittto aliwasuta na 'kuwasunsubika' watekaji. Watu wasiojulikana. Watanzania wanatekwa na kuuawa kama hamna Serikali yenye vyombo vya kuwalinda! Akawaambia Usalama wa Taifa wajitathmini. Akamsuta IGP Sirro kuhusu sinema ya kutekwa Mo Dewji.

Zitto alipiga zote kuhusu mauaji ya Mkiru, yaani Mkuranga, Rufiji na Kibiti. Hakubakisha mauaji ya Uvinza. Safi kabisa, utani wapeleke kwenye vipindi vya maonesho ya stadi zao, siyo katika usalama wa maisha yetu.

Likaja suala la korosho, aisee Zitto hakuikopesha Serikali. Ukweli haipendezi Serikali kudhulumu pesa za wakulima wa korosho na matokeo yake uzalishaji umepungua, vilevile utata mkubwa wa bei umeibuka.

Kula gwala Zitto. Upo ndani ya mioyo ya Watanzania. Wewe ni Mtanzania na unaipenda Tanzania kama Mwalimu Nyerere. Unaipenda haki na kuichukia dhuluma kama Nyerere. Unapenda kupaza sauti kwa ajili ya wanyonge kama Nyerere. Wewe ni mtu wa misingi ya utu, haki za binadamu na utaifa kama Nyerere. Hakika, Taifa hili linapaswa kukutuma ili uitende kazi bora kama lilivyomtuma Nyerere.

Kula gwala mtu wangu.
 
Atari uzi una madini kama yote ivi....Rubi Almasi Dhahabu nk
 
Bange la Njombe au Musoma hilo. Lina mkojo ndani yake.
 
Back
Top Bottom