Kula mbakishie baba

Kula mbakishie baba

mkulungwa02

Senior Member
Joined
May 24, 2020
Posts
193
Reaction score
154
Wana nzengo ngoja niwakumbushe huu mchezo ambao ki ukweli ni moja ya michezo ambayo iliweza kuteka hisia za wengi sana ktk umri Fulani Wa ukuaji wao

Kula kula mbakishie BABA unakuta hapo kuna mchanga halafu katikat kuna kijiti jichanganye sasa ule weeeeee halafu kijiti kianguke wewe ukiwa ndo unakata tonge Walahi kitakacho kukuta hujakuja sahau maisha yako yote

Kuna wengine bana walikua na tabia ya kuwa wakiona mnacheza huo mchezo wanakaa pembeni kusubiri udondoshe kijiti wakushambulie, unakuta mnao cheza ni watu 6 ila ukidondosha kijiti unapgwa na watu 60 hatari sana
 
Tulikuwa na technic . kile kijiti mnakifunga vikamba vingi kwa chini then mnakifukia mchanga mwngi na vile vikamba vinakuwa pande zote za mzunguko wa mchanga ili kuwa wale ambao mwanzoni humega tonge kubwa la mchanga so vile wanajikuta wanapomega wamechukuliza vile vikamba vilivyofungwa na kijiti...

Ngoma inakuja pale umepiga tonge mara paap upepo unavuma na kijiti unakiona taratibu kinadondoka aisee ....

Asa ili usipigwe ukidondosha ni ukimbie na ushike msichana yeyote ndo usalimike.. Kuna kipindi waschana nao walikuwa wanashtuka bas ukianza kuwafukuza nao wanawakimbia kinyama..
 
Kusalimika ilitegemea mmekubaliana vp, wengine tulikuwa tunaweka mti mkubwa ndio rescue point. Sasa mwanza na nawe yake mpaka uufikie huo mti umechubuka magoti.
 
Nakumbuka tukiwa tunacheza huu mchezo, rafiki yetu mmoja ambae alikua bonge (hawezi kukimbia kwa kasi), sasa kijiti kikamwangukia, aisee tulimpiga makofi, hadi mwisho akalala chini, tukaogopa tukijua tumeshaua.
 
Huu mchezo ka hauna nguvu walau uwe na mbio[emoji1787]
 
Mtaji mkubwa wa huu mchezo ni:
1.Mbio
2.Nguvu

Ukikosa kimoja wapo, asavali asavali[emoji38][emoji38][emoji38]. Ila ukikosa vyote ni huruma ya wadundaji tu ndio itakusaidia muda huna hali.

Mimi tabia yangu ilikuwa kuwazibia watu njia wasifike kwenye "rescue tree/point" ambapo mara nyingi tulitumia mti mkubwa ulio zaidi ya mita 10-mita 30 wakati mwingine mpaka mita 50.
Kuna siku nilikamatiwa na mimi nilichezea mpaka kamasi zikatoka. Walinikamata kweli kweli, ila nikapata akili nichane shati, nikawaachia shati waliona vumbi tu...[emoji23][emoji23][emoji23]

Ulikuwa ni mchezo mzuri sana wa kufundishana mbinu za kutoroka mashambulizi, hatari, kwa kutumia mwili ipasavyo, na kuufunza mwili namna ya uvumilivu.
 
Back
Top Bottom