Kulaani Vikali Vitendo vya Kunyanyasa Waumini na Kukandamiza Uhuru wa Kuabudu

Kulaani Vikali Vitendo vya Kunyanyasa Waumini na Kukandamiza Uhuru wa Kuabudu

Kitimoto

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2012
Posts
8,198
Reaction score
9,911
Nalaani hatua yoyote ya Serikali, Taasisi au mtu binafsi anayezuia waumini kuabudu kwa hiari yao ndani ya Makanisa au mahali pengine pa Ibada.

Waumini kuzuiwa kusali katika Makanisa yao ni za kusikitisha, kinyume na maadili yaTtaifa letu na zinakiuka misingi ya haki za binadamu kama inavyolindwa na Katiba.

Uhuru wa kuabudu ni haki ya kikatiba na ya msingi ambayo haiwezi kuvunjwa kwa visingizio vya kisiasa, udhibiti wa mamlaka au sababu zisizo halali. Serikali yoyote inayojihusisha na vitendo vya kuingilia shughuli za kidini, kwa kuzuia sala, kuwatisha waumini au kulifunga kanisa kwa misingi ya upendeleo au chuki, inakiuka hadhi ya utawala wa sheria na demokrasia ya kweli.

Tunaamini taifa imara linajengwa kwa kuheshimu tofauti, kuhimiza uvumilivu wa kidini, na kutetea misingi ya uhuru kwa kila raia. Tunatoa wito kwa wananchi wote kusimama kidete dhidi ya dhuluma ya aina yoyote ile, na kwa viongozi wa dini kutokubali vitisho bali kuendeleza huduma kwa jamii kwa misingi ya imani na maadili.

Wahusika wamelaaniwa wao na kiazi chao milele.

Cc. Pascal Mayalla
 
Wamevunja kabisa kwamba maana walikuwa wanakataa
 
Back
Top Bottom