Kiungo Kimoja tu!
Kwa mwanamke, raha anayopata kutokana na kufanya mapenzi (sex) na mume wake ni muhimu sana katika kukupa faraja na kuendelea kuwa na uhitaji wa sex mara kwa mara na mumeo.
Tafiti nyingi (mfano WebMD, DrPhil) zinaonesha kwamba ni asilimia 50 -75 ya wanawake hawawezi kufika kileleni kwa njia ya kawaida (vaginal stimulation).
Hii ina maana uume kuwa ndani ya uke na kuendelea na misuguano ya kuingia na kutoka kwa kila kona na pembe bado ni vigumu kwa mwanamke kufika kileleni.
Hii haina maana kwamba mwanamke huwa hapati raha ya kimapenzi bali kiwango cha raha (enjoyment scale) ni ndogo ukilinganisha na mwanamke ambaye katika tendo la ndoa huwezeshwa kufika kileleni (orgasm).
Je, siri ipo wapi?
Siri ipo katika kiungo kimoja tu ambacho kinapatikana katika mwili wa binadamu ambapo huwa na nerves nyingi kuliko kiungo chochote katika mwili wa binadamu (mwanaume na mwanamke) yaani kisimi/kinembe/clitoris.
Pia ni jambo linaloshangaza sana kwani kuna wanaume wengi na wanawake wengi (wamo madaktari, mainjinia, wabunge, mawaziri, marais, mashujaa mbalimbali, wachungaji, matajiri, maskini, wanaoishi mijini, wanaoishi shambani, wazungu, waafrika nk) hawaijui chochote kuhusiana na umuhimu wa hiki kiungo katika suala zima ya raha ya sex.
Bottom line ni kwamba wanawake wengi huhitaji kusisimuliwa kisimi/kinembe kwa kila aina ya sanaa (manually & orally) kabla na wakati wa tendo la ndoa ili aweze kufika kileleni.
Mapenzi ni sanaa na kwa kuwa ni sanaa hivyo kuna tips nyingi tu za mke na mume kusherehekea raha ya mapenzi hata hivyo kwa leo tuishie hapa.