Kulea wasiojiweza (Wazee na wale wanaohitaji uangalizi wa karibu) kwa walioopo Hospitalini au Nyumbani. Nipo tayari kuwahudumia

Kulea wasiojiweza (Wazee na wale wanaohitaji uangalizi wa karibu) kwa walioopo Hospitalini au Nyumbani. Nipo tayari kuwahudumia

Care Giver

Member
Joined
Apr 2, 2024
Posts
69
Reaction score
215
Care Giver (Mlezi)
Mimi ni nani?

Mimi ni mtoa huduma ya uangalizi wa karibu kwa wagonjwa au watu wasiojiweza na wanaohitaji uangalizi wa karibu katika kufanya shughuli zao za kila siku.

Huduma hii natoa kwa wagonjwa au wahitaji waliopo majumbani au hospitalini.

MAJUKUMU YANGU NI YAPI?

Kumuogesha na kumuandaa mgonjwa wako.
Kumfulia na kuhakikisha yupo safi muda wote.
Kumvalisha
Kumlisha chakula
Kumkumbusha na kumpatia dawa kama anatumia.
Usaidizi wa kutembea pale anapohitaji.
Kumfanyisha mazoezi ya viungo.
Kumsindikiza hospitali pale anapohitajika kwenda.
Pamoja na majukumu mengine yanayohitaji usaidizi wa mtu.

■Kwa sasa nipo tayari kutoa huduma mkoa wowote ndani ya Tanzania.
Umri - Miaka 34
Uzoefu - Miaka 3
Elimu - Form 4
Jinsia - Kiume

Mawasiliano: 0683 856087

NB
: Naomba share na wanaohitaji huduma hii najua watu wanamajukumu na hapo hapo wanahitajika wa watu wao wanaohitaji uangalizi wa karibu basi hakika suluhisho limepatikana.

Nipo tayari kuwahudumia.
 
Ni wachache sana wenye moyo kama wako si wengine MAneno mengi mixer pombe 24/7 kazi hiyo hatuiwezi hata kdg starehe tatizo
Hakika ni kazi ya kujitoa kweli maana changamoto ni nyingi lakini hatuna budi kuwasaidia ndugu zetu wenye uhitaji pia.
 
Mpo wangapi au utajigawa vipi sababu wahitaji ni wengi na gharama yako ni kiasi gani ?

Naona hapo juu watu wameona huduma wanadhani unafanya kazi ya Kanisa....
Tupo wawili lakini kwa sasa mwenzangu ambaye yeye ni binti tayari ameshapata wakumuhudumia.
Gharama: Tsh 50,000 kwa week
 
Nahitaji huduma Kwa bibi yangu, ila mtoa huduma LAZIMA awe mwanamke, je wew ni jinsia gani?
 
Nahitaji huduma Kwa bibi yangu, ila mtoa huduma LAZIMA awe mwanamke, je wew ni jinsia gani?
Mimi ni mwanaume kwa jinsia ya kike hapana, tupo na mwenzangu mwanamke lakini kwa sasa yupo anaendele na huduma.
 
Tupo wawili lakini kwa sasa mwenzangu ambaye yeye ni binti tayari ameshapata wakumuhudumia.
Gharama: Tsh 50,000 kwa week
24/7 ? Sleep in ?
Kwahio ukishapata moja na kazi inakuwa imekwisha nadhani mgekuwa na agency kabisa ingesaidia sababu hapa ukipata good results wa kwanza akikuchukua tu wa pili anakosa mtu
 
Agency ni kweli wazo zuri lakini tatizo kujitoa kwa baadhi ya watu inakua changamoto mwisho wa siku unaingia mkataba na mtu alafu watu wanakuharibia kazi.
Kwanini nimesema hivyo 50K kwa wiki kwa kazi kama hii ni ngumu sana ndio maana mkiwa na agency hata kidogo kidogo hapa na pale (haba na haba) unaweza kujaza kibaba...; Na watu wakishakuwa wazima wanahitaji saikolojia ya hali ya juu....

Anyway on the bright side huenda hii kazi ya Care ndio the only job ambayo itahitaji Humans huko tunapoelekea nyingine zote zinaweza zikawa automated
 
Back
Top Bottom