Kuleni Tikitimaji (Water Melon) kwa tahadhari

Sie ni wazee wa vice versa, asubuhi chai vitumbua viwili, mchana na usiku ndipo tunapiga milima ya nguvu haswa kumbe kile cha asubuhi ndio kilitakiwa kiwe cha usiku

weka bajeti yako kubwa asubuhi maana baada ya breakfast ndo kazi nyingi na nzito za maendeleo zinatakiwa zikafanyike na sio mchana wala usiku, usiku unahitaji nguvu kidogo tu ya kupapasiana gizani ambayo itabidi pia uilipe asubuhi utakapoamka kwa msosi wa nguvu. Hebu siku moja nenda kaone breakfast ya mchezaji wa Real Madrid au Wayne Rone utakimbia na hutaamini kama ataumaliza huku wachezaji wetu wakila vitumbua viwili na chapati moja wanayodaiwa na Mwina Kaduguda hadi leo, ha.
 
Hilo nalielewa mkuu ila kibongobongo ndio tumelelewa hivyo kiasi kwamba imekuwa mazoea ya kunywa chai na andazi 2 au chapati, huwa ninajitahidi weekend maana katikati ya wiki na mishemishe za kuamka asubuhi unakuta hata muda wa kupata heavy breakfast hakuna waandaaji wamechoka na majukumu ya jana yake
 
kavulata naomba tena maelezo ya hapo uliposema usinywe chai ya maziwa,kwanini tusinywe?
 
Last edited by a moderator:
kavulata naomba tena maelezo ya hapo uliposema usinywe chai ya maziwa,kwanini tusinywe?

everlenk niwie radhi kwa kuchelewa kukujibu kuhusu chai ya maziwa, sijui kama upo kwenye uzi.

Maziwa Maziwa Maziwa!

Maziwa yana protein ya wanyama ambayo kutokana na mchakato wa umeng'enyaji tumboni tumesema unakinzana kwa kiasi kikubwa na mchakato wa umeng'enyaji wa carbohydrates tumboni pia, hivyo haifai kuchanganya tumboni kwako sukari, chapati/vitumbua/bagia/mkate/tambi (CHO) na maziwa (kwenye chai). Hivyo tunashauriwa maziwa yanywewe kama maziwa kwa wakati wake bila kuongezwa sukari wala akina chapati.

LAKINI pia: maziwa yana Calcium nyingi sana na sukari aina ya lactose nyingi. Kwa asili na kwa maumbile ya Mwenyezi Mungu maziwa ni kwa watoto wachanyanga wa binadamu na wanyama wengine wanaonyonyesha (mamalia). Watoto wachanga wanayo miundombinu madhubuti inayowezesha mtoto kunywa/kunyonya, kumeng'enya, kusaga na kufyonza mwilini protein, sukari (lactose) na mazagazaga yote yaliyomo kwenye maziwa kwa urahisi. Miundombinu hii muhimu kwa usagaji wa maziwa inatoweka polepole kadri umri wa mtu unavyoongezeka. Hivyo, Watu na wanyama wakubwa hawapaswi kunywa maziwa hata kidogo maana miili yao imeshapoteza enzymes muhimu (renin) kwa usagaji maziwa tumboni, hatuwezi kuitumia protein iliyoko kwenye maziwa kama walivyo watoto wachanga. Mfano, kati ya watu wazima 10 watakaokunywa maziwa fresh au chai ya maziwa 6 kati yao huwa wataharisha, tumbo kujaa gesi, kunguruma na kuuma (lactose intolerance) muda mfupi baada ya kunywa maziwa kwasababu ya kukosa mmeng'enyo muhimu unaohitajika kumeng'enya sukari (lactose) iliyomo kwenye maziwa.

Mungu hakutengeneza maziwa kwaajili ya watu mazima ila watoto tu, ndio maana anatukomesha tunaokunywa maziwa ya watoto kwa kuharisha, kujaa gesi tumboni na vidonda vya tumbo kwa kunywa maziwa. Wako watu wazembe wanaokunywa maziwa wakizani kuwa maziwa yatawaponya vidonda vya tumbo, huu ni ujinga, usinywe maziwa hata kidogo kama unahisi kuwa una vidonda vya tumbo maana utakiona cha mtema kuni kama una ulcers halafu unakunywa maziwa.
 

somo zuri, barikiwa
 
somo zuri, barikiwa

Powa, somo hili ni gumu kuingia akilini kwakuwa wengi tumekwishazoea kula namna tunavyokula leo. Lakini fanyeni utafiti mdogo tu wa kufuatilia milo na tabia zao za kula watu wenye magonjwa/shida za kansa, pressure, unene kupita kiasi, kiharusi (stroke), kisukari, mafigo, ini, ugumba, na uhanithi. Fuatilia magonjwa ya watu wanaofanya kazi zifuatazo: wauza nyama buchani na machinjioni, supu na nyama choma, mama na baba lishe, wapishi mahotelini, wawindaji porini, wabunge na wafanyakazi wa ofisini na wala nyama maarufu utagundua kitu kinachofanana.
 

hakuna kitu kibaya kama kuishi kwa mazoea, nyakati zinabadilika so kuendelea kung'ang'ania 'eti mababu' walikula hivyo ni hatari zaidi maana nyakati zao na zetu ni tofauti mno.
 
hakuna kitu kibaya kama kuishi kwa mazoea, nyakati zinabadilika so kuendelea kung'ang'ania 'eti mababu' walikula hivyo ni hatari zaidi maana nyakati zao na zetu ni tofauti mno.

Hiyo ni kweli kabisa, tusiishi kwa mazoea, siri kubwa ya afya yako imejificha kwenye vyakula unavyokula, chips/kuku, chips/mayai/nyama choma vitakuletea tu sifa bandia za mahips, matako makubwa, mapaja makubwa, miguu (usafiri) mikubwa, kitambi, shingo kubwa yenye mikunjo lakini afya mbaya mbaya mbaya mbaya kansa, pressure, ugumba, uhanithi kitandani, kisukari, fangasi zisizoisha, allergies, kushindwa kupumua, mafigo, n.k.
 


hiyo yote taabu ya ulimi maana hivyo vyote ni utamu wa ulimini ila kwa afya ni hatari, ukiweza kuushinda ulimi utaishi safi sana, its all abt life style.
 
dhaa mkuu somo ni zuri na pia ni gumu kwel kweli...... natumah wote tuki fata hapa.....tutapunguza foleni hospitalini.......
nini kazi ya naji ya moto mwilini...? I mean kama ukinywa kila Asubuh.....
 
dhaa mkuu somo ni zuri na pia ni gumu kwel kweli...... natumah wote tuki fata hapa.....tutapunguza foleni hospitalini.......
nini kazi ya naji ya moto mwilini...? I mean kama ukinywa kila Asubuh.....

maji ya moto, maji ya uvuguvugu yote heri tu, kila mahali penye joto harakati za kufanyakazi huwa zinaongezeka kuliko pale kwenye baridi kali. Joto linaharakisha na kuongeza speed za mipambano (chemical and physical reactions) mbalimbali tumboni itakayosababisha utumbo "utembee kwa kasi". Hivyo maji ya uvuguvugu yanasaidia kusukuma mbele (speed up) movements za utumbo (peristalsis) na kuharakisha kukisafirisha chakula na makapi ya chakula kutoka kwenye utumbo hadi nje ya mwili. Kitendo hiki kinasaidia mtu kupata choo kikubwa na laini haraka na kuzuia constipation. Lakini pia Kama speed ya kukisukuma chakula kupita kwenye utumbo itaongezeka itapunguza pia muda wa kufyonza chakula mwilini, hivyo kiasi cha chakula kinachotakiwa kufyonzwa kwenye utumbo kwenda mwilini kitapungua, hivyo kuunyima mwili kiasi fulani cha glucose na virutubisho, kitendo hiki cha kukikurupusha haraka chakula bila ya kuruhusu muda mwingi wa kufyonzwa kinaweza kuupunguza uzito wa mtu kwa kiasi fulani.

Maji ya moto pia yanachochea mimeng'nyo tumboni ifanye kazi zake kwa haraka na kusaidia tumbo kumaliza kazi ya kumeng'enya chakula haraka na kuzuia kuvimbiwa.
 

akhsante saana
 
Mama Yang amepata tatizo la figo amembiwa asipate potassium food na fruits naomba ushauri ni matunda gani hayana potassium na vyakula pia.asante
 
Asante sana Kavulata kwa somo zuri. Mm nina tatizo la acid reflux/heartburn,nimetumia dawa za kustop stomach acid production (ppi) but napata nafuu kdg,then hali inajirudia. Naomba nipe meal diet ya tatizo langu. Shukrani!
 
Mama Yang amepata tatizo la figo amembiwa asipate potassium food na fruits naomba ushauri ni matunda gani hayana potassium na vyakula pia.asante

Nimechelewa kukujibu, majukumu yalibana: Pole sana kwa kuuguza mama yako, hakika tatizo la figo linasumbua sana kwa sababu figo ni miongoni mwa viungo muhimu sana kwa uhai wa kiumbe hai. Figo zinalekebisha kiasi cha madini (electrolytes) kinachohitajika mwilini, mafigo yanatathmini na kurekebisha kiwango cha maji mwilini, kutoa uchafu na kuzalisha baadhi ya homoni muhimu saana mwilini, hivyo usicheze na mafigo yako hata kidogo. Mafigo huwa yanakorofishwa na magonjwa ya moyo, pressure, kisukari, kumeza dawa nyingi au dozi kubwa, pombe nyingi, dawa za kujichubua ngozi (kujikoboa) ili uonekane na wewe mashallah japo kwa ngozi ya bandia, heavy metal (mercury, etc.), kunywa maji kidogo kwa siku, n.k.

Dactari aliyemtibu mama yako ninamuamini na nina mheshimu pia kwakuwa yeye amepata bahati ya kumuona, kumsikiliza na kumpima mgonjwa. Ushauri wake ni wa mwisho na muhimu kuliko wa kwangu, nashauri uufuate kwa sasa.

Ila mgonjwa yeyote wa figo lazima ale vyakula visivyo na protein nyingi (protein free diet), potassium kidogo na kuepuka kumpa maji mengi na chumvi (NaCl) nyingi.

Vyakula vilivyo na Potassium viko vingi sana lakini vifuatavyo vina kiasi kikubwa sana: ndizi, machungwa, matango, matikiti, mboga za majani, apple. Fuata ushauri wa ma-dk na wauguzi wake, epuka kumpa dawa za kienyeji ambozo hazijulikani ndani yake kuna nini kwa kiasi gani.
 
Asante sana Kavulata kwa somo zuri. Mm nina tatizo la acid reflux/heartburn,nimetumia dawa za kustop stomach acid production (ppi) but napata nafuu kdg,then hali inajirudia. Naomba nipe meal diet ya tatizo langu. Shukrani!

Lazima ujue kwanini acid inapanda juu ya koo/mdomoni kutoka tumbuni. Je, ni uzalishaji wa acid tumboni umeongozeka (Zollinger–Ellison Syndrome)? Je, ni valves zinazozuia acid kurudi mdomoni zina hitilafu?, je, ni vyakula unavyokula vina acidi nyingi? Unahitaji kugundua kama una vidonda vya tumbo au la. Nenda hospitali ukafanye vipimo kama vile gastroscopy, H. Pylori, barium meal, U sound, etc ili wagundue tatizo lako. Punguza/acha nyama, dagaa, maharage, njegere, maziwa, pombe, sigara, tumbaku, machungwa, apple, ndimu, limau, ukwaju, ubuyu, embe, ndizi bukoba, passionss, mapera, n.k. Pendelea matango, matikitimaji, mboga za majani, tambi,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…