Kuleni Tikitimaji (Water Melon) kwa tahadhari

Kuleni Tikitimaji (Water Melon) kwa tahadhari

Namba 6 mbona mwenyewe unasema 'usipende kula viporo' afu unanishangaa mimi kutokula viporo...je unasoma unachoandika au umekikurupua mahali?

Kumbuka nimesema sili viporo sababu ya knowledge niloipata mahali kuwa si vizuri...wewe ukaanza kuni criticize....sasa hapa na wewe unakubali kuwa si vizuri...

Mimi huwa nasoma side effects na kuzisahau...lakini nachukua conclusion kuwa hiki ni kibaya...viporo ni vibaya...hata kama maelezo nimeyasahau...

Kama wanavyosema sousage ni mbaya...sikumbuki why lakini sili tena sousage...(nakumbuka kidogo kuhusu too much salt...sijui na nini)

Nafurahi na wewe kwakuwa pia uko makini sana. Ni vizuri sana kula vyakula (chakula, matunda, mahindi mabichi, mboga, mikate, n.k) vikiwa vingali fresh, lakini ni vigumu pia kukwepa kula viporo. Mfano, mijini hakuna mashamba hivyo vyakula vingi vinatoka mashambani, itakuwa vigumu sana kwa mtu wa mjini kula matunda, mahindi mabichi, mboga za majani, njegere, n.k vilivyochumwa shambani leoleo, mara nyingi tunakula viporo vya matunda, mboga, mahindi, n.k. ambavyo vimeshaanza kupoteza ubora wake ukilinganisha na watu wa vijijini ambao wanachuma chungwa mtini na kulila hapohapo. Ndioyo maana inafikia watu mjini wanakula viporo vya mahindi mabichi kwa ndimu, chumvi na pilipili. Lakini hata vyakula vingine vinavyopikwa kuna wakati watu wanasafiri mbali hivyo kulazimika kutengeneza vyakula na kusafiri navyo kama viporo, wako watu wasio na muda wa kupika kila wakati kutokana na majukumu yao hivyo kulazimika kupika vyakula na kuhifadhi (preserve) kwenye chupa, jokofu, freezer, chungu, n.k, ndio maana wanashauriwa wavipashe sana moto ili kuua bacteria na fungus kabla hawajavitumia. Viporo havifai sana kwakuwa 1. vinaweza kuchacha na kupoteza ubora wake 2. contaminations kutokana na mavumbi, inzi, mende, n.k ni rahisi 3. radha yake inaweza kubadilika. Kama unamudu kula vitu fresh ni bora zaidi. Hata hivyo watu wengi wa mijini, ulaya na marekani huwa wanakula viporo ndiyo maana biashara ya microwaves na mafriji ni kubwa sana sehemu hizi na ndio sehemu ambazo shida za afya kutokana na vyakula ni kubwa pia. Nilishi Marekani sana, kule ni matajiri tu wanaoweza kumudu kula vitu fresh maana ni ghali sana, wengi wetu tulikuwa tunamudu kula frozen foods na fast foods (take aways) barabarani ambazo hujui ni vyakula vya lini vilivyojazwa mafuta na chumvi nyingi na artificial flavor ili kupoteza harufu ya ukuukuu. Mtu mmoja aliniambia kuwa unaweza kula sausage au samaki aliyewekwa kwenye freezer miaka 6 iliyopita. Ukiweza fanya dada ni bora zaidi.
 
Tumboni kuna madawa makali sana yenye uwezo wa kuunguza na kuua vijidudu, kuchoma kuta za tumbo na utumbo na hata kugandisha maziwa fresh na kugeuka mtindi kwa sekunde chache tu. Kemikali hizi huwa zinazuiwa zisiharibu kuta za tumbo na utumbo na uwepo wa chakula tumboni, bila kuwepo chakula tumboni kemikali hizi zinaweza kuharibu mfuko wa tumbo na utumbo na kusababisha vidonda vya tumbo (ulcers). Hata wazee wa zamani wanalijua hili, ndiyo maana kabla ya kufunga wanaanza kwa kula daku alfajiri ili kuepusha majanga kama hayo, hata hivyo pamoja na kula daku wako watu wengi waliopata vidonda vya tumbo (gastric au duodenal ulcers) kwasababu ya kufunga. Ndo maana hapa mimi nakushauri unywe maji na matunda ili kuukinga ukuta wa tumbo usijekuunguzwe na kemikali kali za tumboni na kupata vidonda vya tumbo.

Nashukuru sana.
 
We kulaaaa vyovyote na chochote lakini ukiona dalili zifuatazo ujue umekosea sana kwenye kula kwako, hivyo badilika au tafuta ushauri haraka:

1. Una tumbo kubwa (kitambi)
2. Una nyama za mwili zinazoning'inia (tumboni, shingoni, kichwani, kwenye mikono na kiwiko, kiunoni, miguuni, mapajani)
3. Kushindwa kupata punzi ya kutosha kutokana na unene
4. Kushindwa kuinama kwasababu ya tumbo kubwa
5. Kukoroma sana ukiwa usingizini kutokana na unene
5. Nguvu za kiume kupungua sana hali ukiwa bado na umri chini ya miaka 60
6. Kukosa nguvu mwilini na kujisikia kiu kupita kiasi - Kisukari
7. Kukojoa sana mkojo mwingi mweupe unaopendwa na sisiminzi - Kisukari
8. Kupata magonjwa ya ngozi hasa fangasi kwenye mapaja, mwilini, kucha, ukeni (mkojo mchafu) kila mara na kujikuna - Kisukari/allergy
9. Miguu kupata ganzi - Kisukari
10. Macho kupoteza nguvu za kuona - kisukari/mafigo/pressure
11. Kukosa usingizi - Pressure
12. Kuwa na wasiwasi, kutoka jasho jingi, mishipa ya shingo kusimama, kuumwa na kichwa - pressure
13. Kihalusi (stroke) - pressure
14. Miguu kuvimba - pressure/mifigo/moyo
15. Mtoto wa jicho - Kisukari/upungufu wa vitamin A
16. kuchelewa kupata mimba ukiwa mnene sana - ugumba
17. BMI zaidi ya 25+ - Overweight
18. Mishipa yako ya damu kupatikana kwa shida - Unene/upungufu wa maji mwilini
19. Kupata choo kigumu - ukosefu wa kula mboga, matunda, kunywa maji, kula vyakula vilivyo kobolewa sana, ukosefu wa mazoezi.
20. Kuvimba mbele ya shingo - Goiter- ukosefu wa madini joto (iodine)
21. Kuchelewa kupona majeraha/vidonda yako - Kisukari
22. Kichefuchefu, chakula hakisangwi tumboni, kuharisha ukila vyakula vya mafuta, macho kuwa ya njano - mafigo/ini/nyongo (bile)
23. Maumivu/sindano kama mchanga kwenye Viungo (joints) hasa vya kidole kikubwa cha mguu, magoti, mikono - gout

....itaendelea......

Heri maskini mwenye afya kuliko tajiri mgonjwa. Kula kidogo ufanye mazoezi kidogo tu kuliko kula sana na kufanya mazoezi makubwa
 
Angalau basi muwe na kumbukumbu ya vyakula mnavyokula kila siku ili kupunguza kula nyama nyama nyama nyama kitimoto kitimoto kitimoto bia bia bia bia bia bia halua halua halua halua soda soda soda soda kila siku kila siku Jumatatu hadi Jumapili January hadi December, kufanya hivyo ni dalili za ujinga kuhusu uhusiano kati ya vyakula na maradhi na ushamba wa kuwa na vijisenti mfukoni. Badilisha tabia kula hovyo ni hatari kwako.
 
Back
Top Bottom