kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
- Thread starter
- #121
Namba 6 mbona mwenyewe unasema 'usipende kula viporo' afu unanishangaa mimi kutokula viporo...je unasoma unachoandika au umekikurupua mahali?
Kumbuka nimesema sili viporo sababu ya knowledge niloipata mahali kuwa si vizuri...wewe ukaanza kuni criticize....sasa hapa na wewe unakubali kuwa si vizuri...
Mimi huwa nasoma side effects na kuzisahau...lakini nachukua conclusion kuwa hiki ni kibaya...viporo ni vibaya...hata kama maelezo nimeyasahau...
Kama wanavyosema sousage ni mbaya...sikumbuki why lakini sili tena sousage...(nakumbuka kidogo kuhusu too much salt...sijui na nini)
Nafurahi na wewe kwakuwa pia uko makini sana. Ni vizuri sana kula vyakula (chakula, matunda, mahindi mabichi, mboga, mikate, n.k) vikiwa vingali fresh, lakini ni vigumu pia kukwepa kula viporo. Mfano, mijini hakuna mashamba hivyo vyakula vingi vinatoka mashambani, itakuwa vigumu sana kwa mtu wa mjini kula matunda, mahindi mabichi, mboga za majani, njegere, n.k vilivyochumwa shambani leoleo, mara nyingi tunakula viporo vya matunda, mboga, mahindi, n.k. ambavyo vimeshaanza kupoteza ubora wake ukilinganisha na watu wa vijijini ambao wanachuma chungwa mtini na kulila hapohapo. Ndioyo maana inafikia watu mjini wanakula viporo vya mahindi mabichi kwa ndimu, chumvi na pilipili. Lakini hata vyakula vingine vinavyopikwa kuna wakati watu wanasafiri mbali hivyo kulazimika kutengeneza vyakula na kusafiri navyo kama viporo, wako watu wasio na muda wa kupika kila wakati kutokana na majukumu yao hivyo kulazimika kupika vyakula na kuhifadhi (preserve) kwenye chupa, jokofu, freezer, chungu, n.k, ndio maana wanashauriwa wavipashe sana moto ili kuua bacteria na fungus kabla hawajavitumia. Viporo havifai sana kwakuwa 1. vinaweza kuchacha na kupoteza ubora wake 2. contaminations kutokana na mavumbi, inzi, mende, n.k ni rahisi 3. radha yake inaweza kubadilika. Kama unamudu kula vitu fresh ni bora zaidi. Hata hivyo watu wengi wa mijini, ulaya na marekani huwa wanakula viporo ndiyo maana biashara ya microwaves na mafriji ni kubwa sana sehemu hizi na ndio sehemu ambazo shida za afya kutokana na vyakula ni kubwa pia. Nilishi Marekani sana, kule ni matajiri tu wanaoweza kumudu kula vitu fresh maana ni ghali sana, wengi wetu tulikuwa tunamudu kula frozen foods na fast foods (take aways) barabarani ambazo hujui ni vyakula vya lini vilivyojazwa mafuta na chumvi nyingi na artificial flavor ili kupoteza harufu ya ukuukuu. Mtu mmoja aliniambia kuwa unaweza kula sausage au samaki aliyewekwa kwenye freezer miaka 6 iliyopita. Ukiweza fanya dada ni bora zaidi.