Kwa wale mliofatilia tukio la kukabidhi hati Ikulu Magogoni kwa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania, mtakuwa mlisikia kuwa Balozi mpya wa Italy nchini ni mbobezi wa masuala ya 'Cyber Security'
Je hii ni diplomatic gesture? Kwamba viongozi wetu wakubwa wameonekana kulalamika dharani 'mambo ya mitandaoni' hasa yule wa Twita. Mawaziri, Wabunge, IGP, Spika, marehemu,wastaafu na Mama sasa hivi kwa nyakati tofauri wamemgusia yule wa kwenye 'Twita' na hivyo kuonesha ni tatizo huku kukiwa na uvujaji mkubwa wa taarifa. Kumekuwa na tetesi za kutumika rasilimali watu, fedha na muda bila mafanikio
Mimi sina ujuzi wowote wa masuala ya kidiplomasia lakini kuletewa Balozi mtaalamu na mjuzi wa masuala ya ulinzi wa mitandao je ni namna ya ku 'offer' huduma kusaidia kutatua matatizo? Kwamba mtu anajua una shida lakini hawezi kuanza kutoa msaada anakuwekea mazingira na kusubiri uombe wewe mwenyewe.
Tukumbuke pia kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa Covid US wametuletea Daktari wa binadamu
Wataalamu wa Diplomasia karibuni