Kuletewa Balozi mtaalamu wa Ulinzi wa Masuala ya Mitandao ni 'Diplomatic Gesture' ?

Umenikumbusha huyu Mzee, kifo chake nakiona ni utata
 
Bwana Lombardi si tu mwanadiplomasia basli ana kazi maalum barani Afrika.

Siku hizi nchi nyingi ziloendelea huleta mabalozi ambao wana upeo mkubwa zaidi na wajuzi wa masuala ya aina tofauti, diplomasia, uchumi, ujasusi na uchumi wa kimkakati.
 
Bwana Lombardi si tu mwanadiplomasia basli ana kazi maalum barani Afrika.

Siku hizi nchi nyingi ziloendelea huleta mabalozi ambao wana upeo mkubwa zaidi na wajuzi wa masuala ya aina tofauti, diplomasia, uchumi, ujasusi na uchumi wa kimkakati.
Tunaweza kufaidika zaidi kwa ujuzi wake mkubwa?
 
Balozi anatakiwa awe na maarifa mengi ili kusimamia maslahi ya taifa lake, hivyo hata Tanzania mabalozi wetu wanaoteuliwa kuiwakilisha Tanzania nchi za nje lazima wawe na ubobezi wa aina fulani kufikia maslahi na malengo ya diplomasia ya kiuchumi.
Mkuu nchi inamteua balozi mwanamitindo au jamaa flani hivi mtoto wa mstaafu, nini maana yako ya mbobezi sasa?.
 
Tukumbuke kuwa Balozi ni mwakilishi kamili wa Rais wa nchi .. hivyo inabidi atoshe vilivyo. huwezi kumwakilisha Rais nusunusu..
hata kauli yako inaweza kusababisha dhahama kidiplomasia.
Kwa mfano Balozi wa Kenya nchini Dan Kazungu amewahi kuwa Waziri nchini kwao.. hivyo nchi zilizo makini hazitumi mtu wa kawaida tu..
 
..Ndio.

..Balozi wa Tz Namibia ni mtaalamu mbobezi wa masuala ya tehama na mitandao.
Yashangaza kuona nchi ina hazina kama hiyo na imeiweka bench la ufundi.
 
Moja ya watu ninaowaheshimu sana humu Jamiiforums, una busara nyingi sana zinafanana na mstaafu wa utumishi wa umma wenye maadili na uzalendo

🙂
Ila mimi si mstaafu bado ni kijana mmoja hivi wa kawaida sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…