Wahenga wanasema "ukimuona Kobe juu ya mti kawekwa" na ukimuona ngedere posta/ kariakoo basi ujue anafugwa.
Ipo hivi kutokana na kelele za upigaji pesa Kama Mo dewji alivyokuwa akiongea pale Simba sc.
Wajanja wa mjini wameamua kutumia indirect way pesa ipite kwa mtu Kisha ijae mahala husika na ndiyo maana akawekwa mtu kivuli (head of scouting).
Nimepitia CV zake kubwa kuliko eti ni shabiki kindaki ndaki wa Simba sc na anaipenda sana Simba kutokana na kuzungumza lugha nyingi uongozi umeona umpe kitengo Cha head of scouting.
Kwa hiyo basi hata shabiki wa Yanga makame Kama angekuwa ana rangi Nyeupe na jinsi anavyoipenda Yanga kila inaposafili na yeye Yupo basi hata makame angelamba kitengo hicho Cha head of scouting.
Hapo nadhani nimeeleweka kwa mfano maridhawa nilioutoa, kuwepo kwa Mels Daalder Simba ni kivuli tu Cha watu wachache kilichochoka kupigiwa makelele kutokana na utafunaji wa Pesa za usajili.
Wanasimba msitegemee furaha, hakuna kilicho badilika.
Nawasilisha hoja.
View attachment 2638967