Kuliko kusubiri kundi kubwa 2028 tuanze Pilot Programme 2027 kwa wanafunzi wa darasa la saba 2026

Kuliko kusubiri kundi kubwa 2028 tuanze Pilot Programme 2027 kwa wanafunzi wa darasa la saba 2026

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
5,503
Reaction score
15,858
Badala ya kusubiri mabadiliko makubwa mwaka 2028, serikali inaweza kuanza mapema kwa kufanya pilot programme kwa wanafunzi wote wa darasa la saba mwaka huu.

Mtoto anayejua kusoma, kuandika na kuhesabu apewe nafasi ya kuendelea kidato cha kwanza mwaka 2027 huku serikali ikifuatilia:

  • uwezo wa shule,
  • matokeo ya wanafunzi,
  • changamoto za walimu,
  • na mafanikio ya mfumo mpya.

Hii itasaidia kupata uzoefu wa mapema, kupunguza watoto kubaki nyumbani, na kuandaa taifa vizuri kwa mfumo mpya wa elimu jumuishi.

Majaribio ya mwaka mmoja yanaweza kutoa majibu bora kuliko kusubiri miaka mingi bila tathmini ya uhalisia.
 
Wangewafanyia wale waliopo Darasa la sita mwaka huu ambao ndio wanatarajiwa kufunga mfumo wa Darasa la Saba mwakani. Maana mwakani kutakuwa na madarasa mawili yanayomaliza Elimu ya Msingi.
Kundi la kwanza ni hilo waliopo Darasa la Sita huu mwaka,na kundi la pili ni waliopo darasa la tano mwaka huu ambao hao kwa mujibu wa mtaala mpya watamaliza elimu ya msingi mwakani wakiwa darasa la sita.
 
Back
Top Bottom