KULIKONI BoT CLUB - ZANZIBAR?.

Musharaf

Senior Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
183
Reaction score
66
Miaka miwili iliyopita, Benki Kuu ya Tanzania tawi la Zanzibar walitangaza tenda ya kutafuta mwendeshaji wa Club yao iliyoko eneo la Mpendae, wakidai watafanya hivyo kila mwaka ikiwa ni utaratibu wao mpya wa kuenzi sheria ya manunuzi ya mashirika ya umma. Baadhi ya wadau walitilia shaka utangazaji wa tenda hiyo wakichelea kuwa huenda ilikuwa ni njia ya kumwondoa mwendeshaji aliyekuwepo awali na kumweka waliyemtaka wao. Naam, wapo ambao husema 'TIME WILL TELL', sasa huu ni mwaka wa pili unaenda wa tatu, hiyo sheria ya manunuzi imeeda likizo au imesinzia?. Itapendeza kama meneja wa tawi la Benki Kuu ya Tanzania Zanzibar atatujuvya hilo.
 
Hizo huduma hapo kwanza ni mbovu kuliko maelezo
 
Na bia zake wala si tamu. Yaani zipo zipo tu.
 
Hii sehemu ipo ipo tu kama ya 1940. Kudaadeki.
 
na bia zake wala si tamu. Yaani zipo zipo tu.
Hivi kumbe na bia huwa tamu,mie nilikuwa najua kuwa bia zote ni chungu?Lakini pia kumbe bia ikiuzwa Rose Garden inaweza kuwa tamu lakini ikiuzwa BOT Club inakuwa sio tamu tena?loh makubwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…