Miaka miwili iliyopita, Benki Kuu ya Tanzania tawi la Zanzibar walitangaza tenda ya kutafuta mwendeshaji wa Club yao iliyoko eneo la Mpendae, wakidai watafanya hivyo kila mwaka ikiwa ni utaratibu wao mpya wa kuenzi sheria ya manunuzi ya mashirika ya umma. Baadhi ya wadau walitilia shaka utangazaji wa tenda hiyo wakichelea kuwa huenda ilikuwa ni njia ya kumwondoa mwendeshaji aliyekuwepo awali na kumweka waliyemtaka wao. Naam, wapo ambao husema 'TIME WILL TELL', sasa huu ni mwaka wa pili unaenda wa tatu, hiyo sheria ya manunuzi imeeda likizo au imesinzia?. Itapendeza kama meneja wa tawi la Benki Kuu ya Tanzania Zanzibar atatujuvya hilo.