Afghanistan
JF-Expert Member
- Dec 18, 2022
- 308
- 403
Habari za Jumamosi wakuu.
Nipo safarini kutoka Dar naelekea mbeya na kesho niunge Border Tunduma katika harakati za uchakarikaji.
Nikiwa naandaa safari yangu lilinijia wazo na nikawaza mengi juu ya safari yangu, pamoja nayo ni usafiri gani nitumie na hoteli gani nikafikie pale Mbeya.
Nikapata jibu kuwa nitatumia usafiri wa basi wakati wa kwenda ila kurudi nitatumia ndege na kuhusu hoteli gani nikifika mbeya nitamtafuta member fulani mdada wa huko anaweza kunisaidia kupata hoteli nzuri kidogo nipumzike hapo walau Siku mbili kisha niendelee na safari yangu mpaka Tunduma.
Sasa changamoto ikaja ni basi gani litanifaa kusafiri nalo ambalo Lina huduma nzuri na halina rekodi mbaya za abiria kunyanyaswa au kuibiwa Mali zao.
Nikakumbuka Kuna jamaa yangu mmoja pale Mbezi terminal aliwahi kuniambia siku za nyuma kuwa nikitaka kusafiri kutumia barabara maarufu ya TAN-ZAM nitumie basi za Sauli au Newforce japo hakudadavua vizuri ni kwa nini na mimi wala sikuhoji Sana kwani nilipata kusoma humu kuhusu ubora wa hizo kampuni mbili.
Hatimaye nikaamua kufanya booking kwenye basi za Sauli na nikapewa tikiti yangu ya kielektroniki tayari kwa safari siku ya Leo .
Cha kushangaza nimefika pale stendi ya Mbezi alfajiri mapema sana kama saa 11 kasorobo hivi lakini sikuona basi lolote la kampuni ya Sauli zaidi Sana niliona wapiga Debe wamevaa t-shirt zilizoandikwa Sauli tu ila Basi sikuona.
Mpaka gari zingine zikawa tayari kwa kuondoka Ile saa 11 ndipo nilipoamua kumfuata Bwana mdogo mmoja ambaye naye alivalia t-shirt iliyoandikwa Sauli nikamuomba anipeleke zilipo ofisi zao, akanipeleka booking office na tukakuta wafanyakazi wengine wapo pale ambapo nilionyesha tikiti yangu. Jamaa mmoja akaichukua na kuikagua, akasema dah kama zali tu maana gari yako ni Ile pale inataka kutoka (akionesha gari ya kampuni nyingine Tofauti na Sauli)
Nikamuuliza inakuaje Nina tikiti ya Sauli na wewe unasema gari ninayotakiwa kupanda ni Ile na haifanani na tikiti niliyokata?unataka kunihangaisha?
Yule jamaa hakuwa na majibu ya kueleweka, nikaona muda unaenda na ananiletea uraia tu ni Bora nipande gari ile aliyonionesha kwani kabla sijafanya booking ilikuwa chaguo la pili ila nilimuonya Sana kuwa nikipata matatizo njiani basi yeye na wenzake walionifanyia mapuuza haya wataubeba Msalaba.
Nikapanda Ile gari safari na mpaka sasa imefikia zaidi ya robotatu hivi ila cha ajabu si barabarani, Msamvu wala Al-Jazeera nilipoona gari yoyote kampuni ya Sauli.
Je, kampuni ya Sauli haipo tena?