Kulikoni bus za Sauli?

Kulikoni bus za Sauli?

Sauli zimejichokea sikuhizi, maana ana bus chache na anapigisha route daily so ana zioverload sana na nyingi ni za zamani ukiacha lile marcopolo G7. Ila kilichomponza na yeye ni kuijifanya anakomaa na mascania tu, kwanza ni gharama ukitaka kununua jipya na running cost yake pia ni kubwa na hayarudishi hela kwa wakati so kuleta bus mpya inakuwa mtihani. Wenzie wanaotumia bus za kichina hizi ziko affordable ndiyo maana kila muda wanaleta bus mpya na mazingira ya ndani unakuta yako vizuri sana yaani very comfortable. Niliwahi kupanda ile Benz DPC 226 nilijuta, gari chafu ndani, seats zimeharibika haribika hovyo, mvua ikinyesha baada ya madirisha yalikuwa yanavuja nikaapa sipandi tena Sauli.
Mtu mwenye gari 7 hawezi battle na mwekezaji mwenye gari zaidi ya 40
 
Na kile kiyoyozi chao kinampiga kelele kama jenereta
AC za Kila siti hakuna.
Seat zinaminya.
Kwa kweli hizi gari zimechakaa sana.
Cha kujivunia kwao kilichobakia ni mwendo tu.
Kama umesafiri karibuni ni kwamba utakubaliana na mimi kuwa Sauli atafurukuta ila kuanzia makambako mpaka uyole unapigwa msako wa mbwa mwizi na new force anafungua geti bila shida
 
Mkuu mtoa hoja Habari,ila naona umeacha maswali mengi kuliko majibu, why ukate ticket ya Sauli na usisafiri na bus hiyo?na ninaichukulia sentence yako kutoka kwa staff wa Sauli aliyekuonyesha bus nyingine with a pich of salt, watanzania wenzangu tuthamini juhudi za wenzetu, elewa watu wanatumia gharama kubwa kujenga brand zao halafu wewe unakuja na upupu huu it's so sad mkuu, why umeenda to low ili iharibu brand ya Sauli?,bus za Sauli zipo na elewa zina royal customer's wake,pls next time do me a favor nenda kapande bus zako za ngamia, na Sauli ya Tunduma to Dar inajaza kila siku (wafanya biashara na ITs driver's)watu wanaokimbiza maisha, mara ohoo mbeya hotel ,mara mwanamke wa JF (humu hakuna prostitute)mara kurudi na ndege sasa kuna watu humu waneshakwea Cathy pacific na wapo kimya, huu ni ukenge sana
Mbona una povu Sana mkuu
 
mmekariri sana tatizo lenu na hizo gari....fika tunduma au kama upo dar nenda ofisi za abood uliza mwaisa anaenda lini tundumaau kama upo tunduma uliza mwaisa anaenda lin lin dar....hizo sauli, sijui new force au golden deer wote wachumba tuu kwa mwaisa.
 
Habari za Jumamosi wakuu.

Nipo safarini kutoka Dar naelekea mbeya na kesho niunge Border Tunduma katika harakati za uchakarikaji.

Nikiwa naandaa safari yangu lilinijia wazo na nikawaza mengi juu ya safari yangu, pamoja nayo ni usafiri gani nitumie na hoteli gani nikafikie pale Mbeya.

Nikapata jibu kuwa nitatumia usafiri wa basi wakati wa kwenda ila kurudi nitatumia ndege na kuhusu hoteli gani nikifika mbeya nitamtafuta member fulani mdada wa huko anaweza kunisaidia kupata hoteli nzuri kidogo nipumzike hapo walau Siku mbili kisha niendelee na safari yangu mpaka Tunduma.

Sasa changamoto ikaja ni basi gani litanifaa kusafiri nalo ambalo Lina huduma nzuri na halina rekodi mbaya za abiria kunyanyaswa au kuibiwa Mali zao.

Nikakumbuka Kuna jamaa yangu mmoja pale Mbezi terminal aliwahi kuniambia siku za nyuma kuwa nikitaka kusafiri kutumia barabara maarufu ya TAN-ZAM nitumie basi za Sauli au Newforce japo hakudadavua vizuri ni kwa nini na mimi wala sikuhoji Sana kwani nilipata kusoma humu kuhusu ubora wa hizo kampuni mbili.

Hatimaye nikaamua kufanya booking kwenye basi za Sauli na nikapewa tikiti yangu ya kielektroniki tayari kwa safari siku ya Leo .

Cha kushangaza nimefika pale stendi ya Mbezi alfajiri mapema sana kama saa 11 kasorobo hivi lakini sikuona basi lolote la kampuni ya Sauli zaidi Sana niliona wapiga Debe wamevaa t-shirt zilizoandikwa Sauli tu ila Basi sikuona.

Mpaka gari zingine zikawa tayari kwa kuondoka Ile saa 11 ndipo nilipoamua kumfuata Bwana mdogo mmoja ambaye naye alivalia t-shirt iliyoandikwa Sauli nikamuomba anipeleke zilipo ofisi zao, akanipeleka booking office na tukakuta wafanyakazi wengine wapo pale ambapo nilionyesha tikiti yangu. Jamaa mmoja akaichukua na kuikagua, akasema dah kama zali tu maana gari yako ni Ile pale inataka kutoka (akionesha gari ya kampuni nyingine Tofauti na Sauli)

Nikamuuliza inakuaje Nina tikiti ya Sauli na wewe unasema gari ninayotakiwa kupanda ni Ile na haifanani na tikiti niliyokata?unataka kunihangaisha?
Yule jamaa hakuwa na majibu ya kueleweka, nikaona muda unaenda na ananiletea uraia tu ni Bora nipande gari ile aliyonionesha kwani kabla sijafanya booking ilikuwa chaguo la pili ila nilimuonya Sana kuwa nikipata matatizo njiani basi yeye na wenzake walionifanyia mapuuza haya wataubeba Msalaba.

Nikapanda Ile gari safari na mpaka sasa imefikia zaidi ya robotatu hivi ila cha ajabu si barabarani, Msamvu wala Al-Jazeera nilipoona gari yoyote kampuni ya Sauli.

Je, kampuni ya Sauli haipo tena?
Aaah poti poti
 
Hi story ilikuwa fupi sana. But imejaa ushamba mwingi. Unaonekana tu hujawahi panda ndege, unataka kumdanganya huyo mwanamke kuwa una pesa. Una ushamba na safari n.k

Sisi ambao hupanda ndege huwa hatuna maelezo mengi kama hayo. Sijui nilitaka kupanda ndege sijui hotel. Ukiingia google ukasearch hotels za mbeya utazikuta na madaraja yake zipo nyingi sana. You dont need to ask. Usiwe unaweka hadharani ushamba wako. Unaaibisha wanaume wengi kwa mpigo.
 
Hii ndefu Sana ngoja nikusaidie

Nilikata tiketi basi la sauli muda wa safar sikuyakuta stand nikaelekezwa gari ingne , je sauli siku hizi hazipo
Mbona umeandika maelezo mengi sana kwa jambo dogo?Ngoja nikusaidie.
..."Nilikata tiketi ya basi la Sauli kutoka Dar kwenda Mbeya.Cha kushangaza nilipofika mapema stendi sikuyaona mabasi hayo.Na badala yake nikaoneshwa magari yenye majina mengine na kuambiwa nipande ili nisafiri nayo.Swali langu:Je,mabasi ya Sauli siku hizi hayapo?"...
 
Sauli alitakiwa awe na bus 16 ili biashara isimsumbue

8 zipaki
8 ziwe njiani, zikifika zinapumzika
Au anunue zhongtong hizo...unapambana na mtu anatumia gari ya kichina vifaa Bei rahisi mafuta haili sana unakuwa unaumia wewe hi ndo ile maswala ya unarusha bomu la dola 10000 kwenye tent ya dola 200 afu unakuta wahuni walishasepa
 
We jamaa kiazi sana.

SAULI umeitaja.
New Force Umeitaja.

Hiyo kampuni nyingine hutaki kuitaja, halafu unalalamika kama Mwanamama.
Unalalamika utafikiri umetoa mbwa vile
 
Ndiyo,
ABC ndilo gari kali Kwa sasa Mbeya, na route hii haina muda sana toka wameanzisha.
Ila ni VIP tu, hakuna semi luxury.

Sauli siku hizi wana mtindo wa kukatia watu wawili siti Moja,
Abiria wanakmjikuta wanagongana kwenye siti na wengine wanaishia kufaulishwa kwenye gari nyingine.
Pia Kwa ndani zimechakaa sana.
Japo mwendo ni uleule.
Heri wewe umegundua huu ukweli
 
Mkuu mtoa hoja Habari,ila naona umeacha maswali mengi kuliko majibu, why ukate ticket ya Sauli na usisafiri na bus hiyo?na ninaichukulia sentence yako kutoka kwa staff wa Sauli aliyekuonyesha bus nyingine with a pich of salt, watanzania wenzangu tuthamini juhudi za wenzetu, elewa watu wanatumia gharama kubwa kujenga brand zao halafu wewe unakuja na upupu huu it's so sad mkuu, why umeenda to low ili iharibu brand ya Sauli?,bus za Sauli zipo na elewa zina royal customer's wake,pls next time do me a favor nenda kapande bus zako za ngamia, na Sauli ya Tunduma to Dar inajaza kila siku (wafanya biashara na ITs driver's)watu wanaokimbiza maisha, mara ohoo mbeya hotel ,mara mwanamke wa JF (humu hakuna prostitute)mara kurudi na ndege sasa kuna watu humu waneshakwea Cathy pacific na wapo kimya, huu ni ukenge sana
Sikuwa na nia mbaya mkuu
 
mmekariri sana tatizo lenu na hizo gari....fika tunduma au kama upo dar nenda ofisi za abood uliza mwaisa anaenda lini tundumaau kama upo tunduma uliza mwaisa anaenda lin lin dar....hizo sauli, sijui new force au golden deer wote wachumba tuu kwa mwaisa.
Shukrani mkuu
 
Back
Top Bottom