Kulikoni ITV kutotangaza habari za Simba SC?

Kulikoni ITV kutotangaza habari za Simba SC?

Jana niliangalia taarifa ya habari ITV, lead story ilikuwa mechi ya IPP na time gani sijui kwenye kombe la NSSF, wakarusha ligi ya zanzibar na kumalizia na mechi ya Manchester. Nilishangazwa sana na kujiuliza kulikoni? Asubuhi wana kipindi kinaitwa kuchambua vichwa vya habari magazetini, ajabu ni kuwa pamoja na kuwa ubingwa wa Simba ulikuwa all over the papers hawakugusia kabisa kuhusu simba.

Nadhani kwa leo wasingekiita kipindi hicho kupitia vichwa vya habari wakati unaacha lead story ya kwenye sports, what a thrash, what a shame ITV.

Kama waligombana kuhusu kurusha mechi live, Simba au timu nyingine yoyote for that matter ilikuwa na haki kukataa, ukionesha mechi live watu wanapungua kuingia uwanjani as a result of which mapato nayo yanapungua. Mechi hizo zinakuwa na wadhamini ambao wanilipa ITV wakati timu hazipati kitu.

Badala ya kuwagomea kuwatangaza, busara ingehitaji ITV na timu za ligi wakae na kuona ni jinsi gani wanaweza kutangaza mechi za ligi ili kuleta faida kwa timu za ligi pamoja na kituo na sio kuigomea timu.

NADHANI HAPO KWENYE NYEKUNDU NDIO UMEIBALANCE HII HABARI, KWA SABABU ASILIMIA KUBWA WALIKUWA UPANDE MMOJA TU! HAYA NI MAMBO YA KIBIASHARA ZAIDI NA TATIZO KUBWA KWA VILABU VYETU NI VIONGOZI AMBAO WAKO KIMASLAHI YAO ZAIDI,
kutatua tatizo ni kwa pande zote mbili kukaa na kuongea Biashara
 
sasa hapo kwenye nyekundu! kama simba walikataa, mbona ITV hawakulalalmika, na Simba wakawaambia sisi hatuna mkataba na nyie, kwa sababu simba walikuwa kibiashara zaidi, sasa iweje ITV wakiwakatalia simba kuwarusha hewani kwa same sababu ya kibiashara iwe nongwa?

kama simba waliweza kufungua gazeti basi wajitahidi na kuweka TV yao, HIZO TIMU ZA SIMBA NA YANGA NI TAJIRI MNO, TATIZO HAWATAKI KUBADILIKA KAMA BADHI YA WATU WA HUMU NDANI
Kituko,
Simba kama viongozi hawajalalamika kwa kitendo cha ITV kususia mechi zao. Ila wanaosema sema sana ni wapenzi na wananchi wa kawaida kabisa kama mimi.

Simba wakiwa na gazeti lao wanaonufaika na habari zile ni wapenzi wa Simba tu, na wafanyabisahara watakaojitangaza kupitia humo.

Lakini kwa ITV kususia mechi kwa mfano ya Simba na Toto Afrika maana yake ni pana zaidi ya ile ya mwanzo (ITV will lose more), na hiyo ndio RAI yangu.

Kuhusu Simba na Yanga kuwa na vituo vyao vya TV, ni wazo zuri ingawa linahitaji mipango endelevu.
 
Nadhani ni mwaka jana au mwaka juzi nilipokuwa huko nyumbani niliwahi kusikia akina Kitenge wanasema kuwa hawatatangaza tena habari za Simba kwakuwa Kaduguda aliwadharau. walikuwa wanawasubiri waombwe msamaha, nadhani hii haikuwa sawa na si sawa kwakuwa habari ni haki kwa mtazamaji na chuki zao haikupendeza kuzileta kwenye vyombo vya habari. hata hivyo bado kuna TV ambazo wafanyakazi wake wako safi km TBC1, Star Tv na Channel 10 tunaweza kupata habari za maana sana kimchezo kuliko kuangalia hiyo channel inayoonesha michezo ya kidali poo na kukimbiza kuku. Achaneni nao!
 
Simba anzisheni TV yenu, hamuoni timu zingine kama Al Hilal, Zamalek na timu za ulaya? kelele tu nunueni airtime!
 
Hii si mara ya kwanza kwa IPP kuichunia Simba habari zake. Ilishawahi kutokea huko nyuma. Inaaminia kuwa kuna ugomvi ulitokea kati ya viongozi wa Simba na watangazaji wa ITV pale Taifa (Shamba la Bibi). Lakini pamoja na matatizo yaliyotokea, uongozi mzima wa ITV unapaswa kuwa na fikra za mbali kibiashara na kimahusiano na wadau wake wa habari, ikiwemo taasisi kama Simba. Athari ambazo zingetokea endapo kama IPP ingejaribu kuzuia magazeti nayo yasiandike habari za Simba, ndizo hizo hizo zinatokea kwenye TV station, japo sio kwa mara moja kama magazeti. Ni kichekesho Simba kuchuniwa na ITV, lakini kuandikwa kwenye Nipashe na The Guardian wakati hao wote baba yao ni mmoja, IPP!!. Sasa kama wao ni chombo cha habari kinachotegemea kuishi kwa kufanya biashara, basi jambo wanalolifanya limepitwa na wakati. Wao kama wafanyabiashara, wangekuwa wakomavu kwa kuchukulia kama ni tatizo la mtu binafsi na sio wao na taasisi. Biashara ni ngumu, na kuna mazingira inabidi "umtafune Jongoo" ili mambo yasiharibike kwako, na sio kukomaa kusiko na ulazima!
 
Totally unprofessional.Kwanza inawanyima watanzania haki ya msingi na ya kikatiba ya kupata habari.Sijui kama inafaa kuitwa media tena hiyo.
 
Nimeshangazwa na kitendo cha ITV kutotangaza michezo ya Simba SC hata kwa tukio kubwa kama la kutwaa ubingwa wa Vodacom Premier League. Nimeambiwa eti wamewanunia viongozi wa Simba kwa sababu waliwakatalia kurusha 'live' moja ya mechi zao. Kwa maoni yangu huo sio uamuzi sahihi. Ni 'very unprofessional', inabidi ITV wajirudi kabla ya kupoteza umaarufu. Watambue kwamba Simba ni klabu kubwa na ina wapenzi wengi ndani na nje ya nchi. Great Thinkers wengine mnalionaje hili?
So what? This is business my friend - it's conducted through a medium called "brain" ...... not "heart".
Anyway, being a supporter from the wrong side of Msimbazi, after failing to see you guys (Simba's) sob on the pitch, what a consolation to see you now cry off it!
 
Nadhani kuna tatizo hapa

Hivi kwanini ITV hawakuendelea kuonyesha mechi zingine? Viongozi wa Yeboyebo walitishia kuishitaki TFF kwa kuruhu mechi zake zioneshwe bila wao kupata kitu sijui iliishaje hii. Kitu ambacho Simba walifanya ni sahihi kabisa na Ndio maana from there hakuna TV yeyote iliyoendelea kurusha Zile mechi live hata Star TV waliacha kuonesha lakini hawajasusia habari za Simba. Ni ukweli usiopingika kwamba vilabu vyetu vinategemea Mapato ya Milangoni na kwa Utaratibu wa Kibongo ukionyesha gemu Live watu wachache sana watahudhuria, sasa hapo club inafaidika vipi?

Mengi ni Yanga Damu na anaumia sana anapoona Simba inafanya Vizuri, hata Kitenge Mwenyewe ni Yanga!

Shauri yao na Roho zao za Korosho, Chuki zao dhidi ya Simba ni Neema za Mafanikio

TV ziko kibao, kuna TBC, Star TV, Channel ten

Ningekuwa Kiongozi wa Simba Ningetoa Wito kwa Mashabiki na Wapenzi wa Simba waachane na ITV

Mtaumia Sana Mwaka Huu,sasa tuone kama hamtatangaza habari ya Gemu yetu na Kandambili

Teh teh teh Nadhani na Siku hiyo kwa Mara ya Kwanza Watasusia Habari za Kandambili
 
Kituko,
Simba kama viongozi hawajalalamika kwa kitendo cha ITV kususia mechi zao. Ila wanaosema sema sana ni wapenzi na wananchi wa kawaida kabisa kama mimi.

Simba wakiwa na gazeti lao wanaonufaika na habari zile ni wapenzi wa Simba tu, na wafanyabisahara watakaojitangaza kupitia humo.

Lakini kwa ITV kususia mechi kwa mfano ya Simba na Toto Afrika maana yake ni pana zaidi ya ile ya mwanzo (ITV will lose more), na hiyo ndio RAI yangu.

Kuhusu Simba na Yanga kuwa na vituo vyao vya TV, ni wazo zuri ingawa linahitaji mipango endelevu.

HAPO KWENYE BOLD NDIPO MNAPOKOSEA, ILI KUPASENI KUUHULIZA UONGOZI WA SIMBA NA WALA SIO ITV, mbona sijasikia mtu akiilalalmikia Dstv, au WAPO au ATN kwamba hawajarusha habari za simba?
 
HAPO KWENYE BOLD NDIPO MNAPOKOSEA, ILI KUPASENI KUUHULIZA UONGOZI WA SIMBA NA WALA SIO ITV, mbona sijasikia mtu akiilalalmikia Dstv, au WAPO au ATN kwamba hawajarusha habari za simba?

Mkuu Kituko Dstv , WAPO au ATN hawajawahi kugoma kurusha Habari za Simba. Hii ya ITV ni Mgomo
 
Mwanzoni walikuwa wanatangaza kwa kuwa walikuwa wanapata maslahi yao kama vile kupitia matangazo ya mechi. Sasa hivi hawatangazi kwa kuwa hawapati maslahi makubwa. Ujumbe huo huo wanaupeleka kwa waandishi wao individually, kwamba kama kuna mshiko (bahasha) leteni habari kituoni itangazwe vizuri. Kama hakuna mshiko (bahasha) msiilete habari kituoni (hata kama ni nzuri). Similarly, this applies kwa habari isiyo nzuri/iliyo mbaya. Kama kuna mshiko basi utolewe ili habari mbaya isitangazwe, kama hakuna mshiko basi habari mbaya itatangazwa. So, generally wanatupa picha kwamba maslahi binafsi kwanza, halafu baadaye maslahi ya taifa (kama wakipenda). HII NI RUSHWA kwa kuwa mwandishi/kituo cha matangazo hakiwajibiki equally eti kwa kuwa kilinyimwa fursa ya pesa!

FANI YA HABARI IMEVAMIWA....HASA NA MDUDU "fisadi wa elimu" NA NDUGU YAKE .."bahasha za kaki"(RUSHWA) Na habari zisizo za kiuchunguzi........!a.k.a udaku.Unakuta habari inageuzwa kwa matakwa ya "mtoa posho" na si habari kama habari.Kwa sasa ukitaka mtu atolewe kwenye zee komedi you just contact those guys with something in your hand! watamflash mpaka kweli atapakae uchafu mbele ya jamii....!Take an example of MAMA MMOJA 9mke wa mheshimiwa)ALIYEFIKISHWA MAHAKAMANI HIVI MAJUZI NA ZEE KOMEDI KUMRUSHA HEWANI......THE REAL STORY IS VICE VERSA FROM WHAT THE TANZANIA MEDIA IS BRINGING TO THE PEOPLE...! WANASEMA MAMA HUYO NI TAPELI..WHILE THE ONE ACCUSING HER NDO ALIYEYEFANYA SO HILO NA KUGEUZA KIBAO KWA MAMA YULE .....wangekuwepo waandishi wa habari za uchunguzi BLACK AND WHITE OF YHE STORY COULD BE OUT......!LAKINI MEDIA ZETU,NOT ONLY ITV NA NIPASHE KUTOHABARISHA UMMA HABARI ZA SIMBA S.C ZIMEJAA RUSHWA NA KULINDA WAHALIFU....!MTU HUYO TAYARI ANA KESI ZA KUTOSHA ZA UTAPELI MAHAKAMANI HAPO HAPO...NA TAYARI YEYE NDO ALIYERIPOTIWA....(AS USUAL @ POLICE STATIONS MAMA MH. WAS SENT TO COURT INSTED OF THE FAMOUS TAPELI KIMAMB....!MEDIA MEN CHANGE TO BRING HOPE TO THE PEOPLE.....MTAFANYA NISADIKI KAULI YA KIONGOZI MMOJA WA AWAMU ILIYOPITA KUWA HASOMI/HAFUATILII MAGAZETI YA KIBONG
 
Kwa kweli hawa jamaa wana udhaifu mkubwa. huwa nashangaa wanatangaza matokeo ya mechi za mchangani lakini wanaacha kutangaza matokeo ya mechi za ligi kuu iwapo wekundu wamecheza.kwa namna yoyote ile hawatendei haki watazamaji wao
 
Nimeshangazwa na kitendo cha ITV kutotangaza michezo ya Simba SC hata kwa tukio kubwa kama la kutwaa ubingwa wa Vodacom Premier League. Nimeambiwa eti wamewanunia viongozi wa Simba kwa sababu waliwakatalia kurusha 'live' moja ya mechi zao. Kwa maoni yangu huo sio uamuzi sahihi. Ni 'very unprofessional', inabidi ITV wajirudi kabla ya kupoteza umaarufu. Watambue kwamba Simba ni klabu kubwa na ina wapenzi wengi ndani na nje ya nchi. Great Thinkers wengine mnalionaje hili?
What's Simba SC?!! 😱😱😕😕
 
Mkuu Kituko Dstv , WAPO au ATN hawajawahi kugoma kurusha Habari za Simba. Hii ya ITV ni Mgomo

swali la maana kabisa hapo ni kwanini ITV wagome kurusha habari za simba, ukiijua sababu ndio utakuwa kwenye position ya kuwalaumu ITV
 
Totally unprofessional.Kwanza inawanyima watanzania haki ya msingi na ya kikatiba ya kupata habari.Sijui kama inafaa kuitwa media tena hiyo.

Una mawazo mgando leseiyo, dunia ya sasa inaendeshwa kibiashara zaidi. Umetolewa mfano mzuri wa TFF na Dstv pamoja na GTV, Channel 10 na magazeti ya IPP.

Kama bado uelewi mwelekeo wa dunia ya sasa omba msaada. Mbona ujiulizi mbona Dstv wanatangaza matokeo ya mech za Kenya Premier League na wakati za Tanzania hazitangazwi??
 
Kwa kweli hawa jamaa wana udhaifu mkubwa. huwa nashangaa wanatangaza matokeo ya mechi za mchangani lakini wanaacha kutangaza matokeo ya mechi za ligi kuu iwapo wekundu wamecheza.kwa namna yoyote ile hawatendei haki watazamaji wao

Nikisoma michango kama hii huwa nacheka sanaaaa......poleni watanzania, najua wengi bado mmefunikwa na fikra za Azimio la Arusha!!

Stuka......karne ya sasa watu wako kibiashara zaidi na maslahi binafsi!!
 
Wanasimba bana mbona mnakuwa wavivu wa kufikiri ITV yenu hiyo? Mbona kuna habari utakuta zinatangazwa ITV lakini kule TBC hakuna au StarTV jamani mmeanza choko choko au ndo mnatafuta sababu ya kipigo cha tar.11? Lipieni basi kipindi maalumu mrushwe kama mna hela/.
 
Kuna siku simba walicheza na ruvu, nilitamani sana kujua mchezo ulikuwaje na matokeo kwa ujumla.......nimeganda nasubiri habari za michezo ITV....hawakutangaza. Toka siku hiyo habari za michezo naangalia Star TV. Uchambuzi wao naupenda pia maana ni wa kina.
 
Back
Top Bottom